Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimetembelea mikoa yote ya Tanzania na karibu wilaya zote isipokuwa chache tu zisizozidi saba....Aisee Tanzania kuna maeneo mengi mazuri...Mufindi, Lushoto na kadhalika...Lakini jamani kuna kaeneo au kamji ambako mtu huwezi ukaamini kuwa ni kazuri hako ni Kahama...dah, napapenda sana pale.
 
HAPO Kagera ni wilaya zote kuanzia
Ngara,Muleba,biharamulo,Bk Rural and Urban na hata karagwe maaeno ya Nyakahanga,Mulushaka etc pote nilichafua.
Enzi nasaka Kahawa na ndizi nazisafirisha ki Magendo..
Nilikuwa sipendi ile pombe yao ya Ndizi.

Tukija Njombe Kule town maeneo ya kuazia Ramadhani,hagafilo,Chaugingi,Kibena,Uzunguni,Tanwat pote Nilikanyaga WAKATI tunasaka madalali wa mashamba ya mbao.
kule lupembe Na matembwe karibu na Shule ya manyunyu niliruka Sana na pipoz za Kule daah Enzi tunaenda lupembe kusaka maparachichi na kuyasafirisha nje.
Tumelangua Sana mpaka tukapata mashamba ya maparachichi kule.

Kufika maeneo ya makambako tulikuwa tunafanya udalali,na kuuza vitu coz makambako ilikuwa Ni centre ya wafanyabiashara karibu wa kusini.

Tukija Iringa daah.
Sitopasahau kule pagawa na maeneo ya mtandika lukosi,
maisha ya kulima vitunguu yalikuwa magumu na full ushirikina.

hapo Morogoro,Dar,Tanga na Pwani sisemi maana naendaga ZAIDI navyokwenda msalani.

Tour Ambayo Nili enjoy Ni ile niliyozunguka mikoa ya Kusini
Kule pesa Ngumu lakini people's za Kule bado hazijajanjaruka ilikuwa Ni full kuwalaghai.

mkoa wa Kigoma sikuupendelea Sana
coz ya wingi wa wakimbizi na muingiliano wa warundi,wacongo na waha
hahahaha utaomba pooo

Wewe mleta maada umezunguka mikoa less than 5 .Kati ya mikoa 30?!

bado SANAA

Kwa Sasa naisaka njia ya Tunduma kutokea Momba




Sent using Jamii Forums mobile app
huwez kuisimulia vzur njombe na fursa zake bila kusahau mbao, matunda na mazao ya chakula km mahindi na maharage


karbun xn njombe

babawawili
 
Ndo maana usafiri wa meli ulikuwepo Sana kipindi hicho.mv bukoba ,mv kipepeo,mv kishimba na mv Victoria zote zilifanya safari ya Bukoba mwanza.bukoba ilikuwa kama kisiwa kipindi hicho ndo maana tabia za huko na tamaduni zao ni tofauti Sana na watz wengi


Sent using Jamii Forums mobile app
Eatu wa bukoba huwa wanadharau wageni.niliona kwa mda mchache nilipokiwa pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barabara pasua kichwa ile.Hivi inawezekana vipi miaka zaid ya 50 ya uhuru.barabara inayounganisha mkoa na mkoa haina rami.alafu inakera ni vile full mbuga
Mpanda panatia simanzi,kila nikipata trip ya kwenda Katavi naifikiria sana barabara ya Tabora to Mpanda.

Never say never

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAPO Kagera ni wilaya zote kuanzia
Ngara,Muleba,biharamulo,Bk Rural and Urban na hata karagwe maaeno ya Nyakahanga,Mulushaka etc pote nilichafua.
Enzi nasaka Kahawa na ndizi nazisafirisha ki Magendo..
Nilikuwa sipendi ile pombe yao ya Ndizi.
Tukija Njombe Kule town maeneo ya kuazia Ramadhani,hagafilo,Chaugingi,Kibena,Uzunguni,Tanwat pote Nilikanyaga WAKATI tunasaka madalali wa mashamba ya mbao.
kule lupembe Na matembwe karibu na Shule ya manyunyu niliruka Sana na pipoz za Kule daah Enzi tunaenda lupembe kusaka maparachichi na kuyasafirisha nje.
Tumelangua Sana mpaka tukapata mashamba ya maparachichi kule.
Kufika maeneo ya makambako tulikuwa tunafanya udalali,na kuuza vitu coz makambako ilikuwa Ni centre ya wafanyabiashara karibu wa kusini.
Tukija Iringa daah.
Sitopasahau kule pagawa na maeneo ya mtandika lukosi,
maisha ya kulima vitunguu yalikuwa magumu na full ushirikina.
hapo Morogoro,Dar,Tanga na Pwani sisemi maana naendaga ZAIDI navyokwenda msalani.
Tour Ambayo Nili enjoy Ni ile niliyozunguka mikoa ya Kusini
Kule pesa Ngumu lakini people's za Kule bado hazijajanjaruka ilikuwa Ni full kuwalaghai.
mkoa wa Kigoma sikuupendelea Sana
coz ya wingi wa wakimbizi na muingiliano wa warundi,wacongo na waha
hahahaha utaomba pooo
Wewe mleta maada umezunguka mikoa less than 5 .Kati ya mikoa 30?!
bado SANAA
Kwa Sasa naisaka njia ya Tunduma kutokea Momba
Sent using Jamii Forums mobile app
PAWAGA ndilo jina halali si Pagawa! Kweli ulipagawa.
 
Mbeya, Uporoto kama ulaya vile baridi lake, Tukuyu na Kyela kuzuri hakuna mfano, mashamba ya miti, pareto, migomba, chai, kahawa, michikichi, korosho, kokoa na kila zao unalolijua lipo huko, kunapendeza sana.
 
Hamjajua tu wadogo zangu,,,,,,,mkoa Wa ajabu kuliko yote hapa bongo ni mbeya.....nilifika huko nikaishi kama miaka mi NNE.

Jamani ule mji ukiachana kabisa na pale mbeya mjini, yani kila sehemu panavutia kuishi na kila mji uliopo ndani ya ule mkoa umechangamka mpka nikawa nashangaa...

Mkoa wa mbeya ulinivutia sana kuliko mikoa yote niliotembea.......
Arusha na Moshi ni mikoa mizuri tu kimuonekano Wa juu juu na mandhari zake pale mijini lkn ukiingia ndani ndani hali zinatisha......na kusema ukweli ni mikoa ambayo ili uweze kuishi pale basi lazima uwe ni mtu Wa kipato kizuri sana.

Lakni Kule mbeya kwa wanyakyusa,wasafya, wanyiha wandali na wakinga ndugu zangu unaweza kuishi hata kama ni MTU Wa kuingiza Tsh 3000 tu kwa siku katika biashara zako.

Hali ya hewa ni nzuri na ina alternate..(Joto kiasi kwa kipindi flani na baridi ya mizuka kwa kipindi flani)

Kuhusu ardhi hilo ndo halina ubishi,,,,,,hata mazao karibu yote yanakubali kule Mbeya.

Mji umejengeka in some extent inaridhisha.

Shida ni moja tu mbeya.......

VIJANA WA KULE NI WAKOROFI SAAAAAAANAAAA YANI SAAANAAAA.........tena wote,,,,akuna cha mbeya mjini sjui tukuyu wala kyelaa au mbozi tunduma....yani ukorofi ni kama jadi yao na ma overconfidence ya ajabu ajabu...

Na lugha zao za asili wanaziongea kinoma kuliko kawaida.......!!!!

Mi ni mzaliwa Wa Tanga Handeni.
Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbeya kwetu pako vizuri sana. Handeni kwenu nimeenda mara ya kwanza miez miwili iliopita. Ni mji mzuri umechangamka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom