Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Nimezunguka mikoa karibu yote kasoro Kigoma na Zanzibar....
Kwangu mbeya na mwanza palinivutia....
Mji.unaokua taratibu ni sumbawanga, tanga na ruvuma....
Mkoa wenye barabara hatari ni ruvuma kuanzia kuingia mpk ukanyage mbamba bay mpaka tunduru ni kona za hatari....
Hivi mpanda itakumbukwa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimetembea karibu robo tatu ya nchi ,ukiacha mara,kigoma,mtwara,lindi na kagera..sehemu iliyonivutia ni arusha,njombe na Ifakara unfortunately naishi sumbawanga ni kuzuri wadada wazuri ila mzunguko wa pesa mdogo na ukuaji wa mji ni slow sana yaani hata kimapato ya mkoa mwaka uliopita ilikua ya mwisho kitaifa
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
karibu sana Lushoto mkuu,my home land
 
Interesting
Kwa kifupi nimezunguka Tanzania nzima, nimefika mikoa yote isipokua Pemba tu!

Safari yangu ndefu kuliko zote nilisafiri km 7300. Safari Ilianzia Dar, Lindi, Mtwara, Songea hadi Biharamulo, Njombe (Rudewa, Rujewa, kule kwenye Baridi Sana), Makambako, then Mbeya, Kyela, na kule juu Chunya, Then Tunduma, Sumbawanga: Mtowisa-Ziwa, Kaburi wazi, Wampembe, Namanyere Nkasi, Mwimbi, kwingine Majina magumu nimesahau. Toka hapo nikaenda Katavi na Wilaya zake, then Tabora, kutoka Tabora nikaenda Kigoma na Wilaya mbili, nilifika hadi Karago, kwenye Wakimbizi then Biharamulo nikalala hapa, nikaenda Bukoba then Mwanza, Kutoka Mwanza nikaenda Simiyu hadi Kishapu, nikarudi kulala Shinyanga na kupumzika kidogo then nikarudi Singidani na Wilaya tatu hadi Itigi, Manyoni kisha nikarudi Dodoma hadi pale ambapo wale watafiti walichomwa Moto miaka Ile.

Dodoma nikapita njia ya Kati hadi Iringa kwenye mashamba ya chai kule hadi kile kijiwe kinaitwa Makei pale kwenye mbao then tukarudi Dar. Ilikua Safari nzuri saaaana na ngumu saäana. Sitakaa nisahau Daima. Ngoja nitafute picha baadhi niweke

You are strong than what you think...
 
Sio Mulushaka wewe... Ni Omurushaka.
Na makao makuu ya wilaya ya Karagwe ni Kayanga. Sio nyakahanga...
Hujaitaja Misenyi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona unanisingizia
wapi nimesema kuwa hayo Maeneo Ni makao makuu ya karagwe?
Kule nyakahanga si ndiyo Kuna na hospital kubwa ya mji?

hayo majina yenu mnatamka ki lafudhu za kinyambo na hata Mimi Ni mswahili wa Pwani nitajulia wapi?
nimeliandika neno the way nilivyokuwa nalitamka
Mambo ya kusema omuru nin siyawezi me

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapenda milima wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Umenikumbusha miaka ya 2000 nikiwa Dodoma nilikuwa na jamaa yangu kwao Bukoba, likizo anaondoka Dodoma hadi Dar na Scandinavia Express, anachukua Akamba hadi Kampala kupitia Nairobi, halafu anaingia Bukoba ...yote hiyo kukwepa barabara kipande cha Dodoma mpaka Bukoba maana kilikuwa vumbi na ujambazi kwa wingi
 
Nimetembea karibu robo tatu ya nchi ,ukiacha mara,kigoma,mtwara,lindi na kagera..sehemu iliyonivutia ni arusha,njombe na Ifakara unfortunately naishi sumbawanga ni kuzuri wadada wazuri ila mzunguko wa pesa mdogo na ukuaji wa mji ni slow sana yaani hata kimapato ya mkoa mwaka uliopita ilikua ya mwisho kitaifa
Hivi we ni mkenya au mbongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha miaka ya 2000 nikiwa Dodoma nilikuwa na jamaa yangu kwao Bukoba, likizo anaondoka Dodoma hadi Dar na Scandinavia Express, anachukua Akamba hadi Kampala kupitia Nairobi, halafu anaingia Bukoba ...yote hiyo kukwepa barabara kipande cha Dodoma mpaka Bukoba maana kilikuwa vumbi na ujambazi kwa wingi
Ndo maana usafiri wa meli ulikuwepo Sana kipindi hicho.mv bukoba ,mv kipepeo,mv kishimba na mv Victoria zote zilifanya safari ya Bukoba mwanza.bukoba ilikuwa kama kisiwa kipindi hicho ndo maana tabia za huko na tamaduni zao ni tofauti Sana na watz wengi


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom