Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Kama wewe.ni mwanaharakati wa maisha huwezi kuwaza ngono au wanawake wazuri.
Wanawake wazuri ulikuwa unawapata baada ya kumaliza harakati na kuvuna mawe then unaenda home au kambi yako kujipumzisha

HAKUNA Raha kama kuwa mwanaharakati smart and G.Man.
Tulikuwa team ya vijana Kama 5 ambao tulitoka dsm na tulijuana kupitia humu Jf na WhatsApp Group.

Lengo ilikuwa kusaka Fursa kwa udi na uvumba mikoa yote ya Tz

Kwenye Team yetu wawili walikuwa wazee wa starehe na mijimama wao walikuwa full kuchafua.
Walikuwa wanatupa shida kwenye baadhi ya vijiji coz ya ushirikina waliokuwa wanafanyiwa kwa Mambo yao.
Lakini pia walikuwa Wana TU cost Sana.
tunaweza fikia town tukapanga SAA 10 alfajiri tuanze safari ya kwenda maporini
Sasa wao walikuwa wanafikia pombe na starehe akirudi SAA 8 usiku yupo na Pombe Kichwani ukimuamsha morning hapo utakuwa mzozo.
walikuwa wanaturudisha Nyuma Sanaa.

Sisi wengine tulikuwa tuna spend na wazee, ndugu na mpenzi as wife material
hapo pesa,ilikuwa inaonekana bila shida.

daah Tz Kuna Fursa Sana kuliko sehemu yeyote ile duniani

Shida vijana wengi Wamelala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro mi nikijana naependa kujishighulisha naomba unitajie fursa mbalimbali ulizoziona kwa kuzunguka kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado kufika katavi na pemba tu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ni Mbuga ya Katavi ukitokea Sumbawanga! Hapo Nilikua Naitafuta Katavi moja, kuna mbung'o balaa
IMG_20161022_113800.jpeg


You are strong than what you think...
 
Hongera Sana, nimefika Handeni Mara nyingi nikielekea Wilaya mpya....
Hamjajua tu wadogo zangu,,,,,,,mkoa Wa ajabu kuliko yote hapa bongo ni mbeya.....nilifika huko nikaishi kama miaka mi NNE.

Jamani ule mji ukiachana kabisa na pale mbeya mjini, yani kila sehemu panavutia kuishi na kila mji uliopo ndani ya ule mkoa umechangamka mpka nikawa nashangaa...

Mkoa wa mbeya ulinivutia sana kuliko mikoa yote niliotembea.......
Arusha na Moshi ni mikoa mizuri tu kimuonekano Wa juu juu na mandhari zake pale mijini lkn ukiingia ndani ndani hali zinatisha......na kusema ukweli ni mikoa ambayo ili uweze kuishi pale basi lazima uwe ni mtu Wa kipato kizuri sana.

Lakni Kule mbeya kwa wanyakyusa,wasafya, wanyiha wandali na wakinga ndugu zangu unaweza kuishi hata kama ni MTU Wa kuingiza Tsh 3000 tu kwa siku katika biashara zako.

Hali ya hewa ni nzuri na ina alternate..(Joto kiasi kwa kipindi flani na baridi ya mizuka kwa kipindi flani)

Kuhusu ardhi hilo ndo halina ubishi,,,,,,hata mazao karibu yote yanakubali kule Mbeya.

Mji umejengeka in some extent inaridhisha.

Shida ni moja tu mbeya.......

VIJANA WA KULE NI WAKOROFI SAAAAAAANAAAA YANI SAAANAAAA.........tena wote,,,,akuna cha mbeya mjini sjui tukuyu wala kyelaa au mbozi tunduma....yani ukorofi ni kama jadi yao na ma overconfidence ya ajabu ajabu...

Na lugha zao za asili wanaziongea kinoma kuliko kawaida.......!!!!

Mi ni mzaliwa Wa Tanga Handeni.
Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app

You are strong than what you think...
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi mpaka mafia sehemu ambayo sijafika ni pemba na ukerewe tuu
 
Nimezunguka mikoa mingi nimeona sehem zenye lodge nzuri za kueleweka kwa Bei nafuu Ni
MASASI..HUU MJI MZURI KUPITA MKOA WAKE MTWARA
GEITA..PA UKWELI SANA
UNA MAANISHA MASASI PAZURI KULIKO MTWARA MJINI AU SIO??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom