Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Write your reply...mimi nilipenda wakinga Wa makete tuu n.a. zile Taa zai za mbinguni usiku
Makete hii mwaka juzi Wakati wanajenga Barabara
IMG_20180225_112951.jpeg


You are strong than what you think...
 
Nimetembelea na kuishi mikoa ifuatayo

Mtwara
Lindi
Ruvuma(Tunduru na songea ,namtumbo)
Arusha
Kilimanjaro
Tanga
Pwani
Dar
Kigoma
Simiyu
Mara
Manyara
Singida
Dodoma
Tabora
Geita
Mwanza (ndo naishi now)
Morogoro

Sijawahi kukanyaga
Kagera
Pemba
Zanzibar
Iringa
Mbeya
Katavi
Rukwa

Ila lazima nifike tu kwenye hii mikoa

Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOTE

Karibu Sana mkuu-Mbàlizi,Mbeya!
 
Kama mtu niliyeishi Iringa na Dodoma at some point my life, its laughable unavyousifia mji wa Iringa against Dodoma. Hata kabla serikali haijaamia kibabe.

Na nimekomenti kama mtu ninayepapenda Iringa sana.
Pazuri, ila usipa-exaggerate hivyo.



Sent using LF Electromagnetic Waves
 
Hii ni Kilindi Mkoa wa Tanga.... Ukitaka kupata video Ingia YouTube tafuta Surfing Tanzania
FB_IMG_1554752609586.jpeg


You are strong than what you think...
 
Mimi chalinze pale msolwa watu walinipenda sana wake kwa waume watoto wazee na vijana

Sehemu ya pili ni buseresere katoro geita kule maisha raha sana pesa ipo bata zipo na watu wana roho zao nzuri kama sura zao
Khaaa kumbe geita Wana karoho kazuri zuri nilikuwa sijui
 
nilipaelewa sana iringa miami pub &luxury pub
mbeya mafiat- savoy guest and bar
songwe- kitelewas pub
misungwi- ndinga bar
mwanza-bundesliga,diamond
dom-mwanga bar,chako ni chako
singida-rwezaura,kirima
zenji-gymkhana,masingini,police mess,nyuki,gofu,kianga kwa mbawala,aman fresh,tunduni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! Karagwe is my home town, pale mitaa ya Kayanga!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom