Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Tanzania ni kubwa sana aisee..kuna chaka ukienda huwezi amini fursa zilizopo..tatizo miundombinu bado ni changamoto kwa baadhi ya maeneo..ila inahitaji roho ngumu na kuweka pembeni starehe maana kwanza mazingira mengine hayana hata sehemu useme uende uoshe macho sehemu.
Aisee
 
Nimebakiza Sumbawanga, Kigoma, Kagera, Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Pemba...

The rest nmeshapita...


Aiseee Mwanza na Tanga ni mikoa the best kwangu....
 
Bkb..mwz..tbr..singida..dodoma..moro..dsm..pwani..tanga..arsh..klinjaro..lind..mtwara..njombe..iringa..shinyanga..simiyu..geita..kigoma..nimefika huko kote.

Mwaka huu mwishoni ntaenda zenji..nikajichukulie vimwali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kayanga pako poa sana, nimekaa kwa muda na mazingira yake niliyapenda sana, hakika Tanzania ni nchi nzuri sana.
Wakati nakwenda Karagwe nilipadharau sana lakini nilipofika niliopna papo poa tu na nilikaa miaka 2 hivi kipindi hicho mitandao ya simu ndio ilikuwa inaingia na nikakuta kuna watu wa Cable (Kabunga) yaani mpaka Super Sport ipo nacheck game nikiwa ndani wakati Dar na sehemu zingine wanakomaa kwenye vibanda umiza
 
Pamoja na umri huu nimetembea mikoa 6 tu na sitarajii kuongeza.
 
Nimezunguka mikoa karibu yote kasoro Kigoma na Zanzibar....
Kwangu mbeya na mwanza palinivutia....
Mji.unaokua taratibu ni sumbawanga, tanga na ruvuma....
Mkoa wenye barabara hatari ni ruvuma kuanzia kuingia mpk ukanyage mbamba bay mpaka tunduru ni kona za hatari....
Hivi mpanda itakumbukwa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Songea to mbamba bay kupo ok kwasasa
 
Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es salaam, Morogoro, dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, na Tanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom