Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Interesting
Kwa kifupi nimezunguka Tanzania nzima, nimefika mikoa yote isipokua Pemba tu!

Safari yangu ndefu kuliko zote nilisafiri km 7300. Safari Ilianzia Dar, Lindi, Mtwara, Songea hadi Biharamulo, Njombe (Rudewa, Rujewa, kule kwenye Baridi Sana), Makambako, then Mbeya, Kyela, na kule juu Chunya, Then Tunduma, Sumbawanga: Mtowisa-Ziwa, Kaburi wazi, Wampembe, Namanyere Nkasi, Mwimbi, kwingine Majina magumu nimesahau. Toka hapo nikaenda Katavi na Wilaya zake, then Tabora, kutoka Tabora nikaenda Kigoma na Wilaya mbili, nilifika hadi Karago, kwenye Wakimbizi then Biharamulo nikalala hapa, nikaenda Bukoba then Mwanza, Kutoka Mwanza nikaenda Simiyu hadi Kishapu, nikarudi kulala Shinyanga na kupumzika kidogo then nikarudi Singidani na Wilaya tatu hadi Itigi, Manyoni kisha nikarudi Dodoma hadi pale ambapo wale watafiti walichomwa Moto miaka Ile.

Dodoma nikapita njia ya Kati hadi Iringa kwenye mashamba ya chai kule hadi kile kijiwe kinaitwa Makei pale kwenye mbao then tukarudi Dar. Ilikua Safari nzuri saaaana na ngumu saäana. Sitakaa nisahau Daima. Ngoja nitafute picha baadhi niweke

You are strong than what you think...
Baadhi ya picha
IMG_20170213_124600.jpeg
IMG_20170214_142259.jpeg
IMG_20170209_104425.jpeg
IMG_20170205_155540.jpeg
IMG_20161019_154221.jpeg
IMG_20161227_125330.jpeg
IMG_20161019_153844.jpeg
2013-04-28%2011.32.57.jpeg
IMG_20161019_154221.jpeg


You are strong than what you think...
 

Attachments

  • DSC_0098.JPG
    DSC_0098.JPG
    88.5 KB · Views: 27
Kittalu in acho 2acres bei20'000 mlion maelewano yapo
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanza, Sengerema, Geita, Katoro, Bmulo, Masumbwe, Ushirombo, Misungwi, Shinyanga, Nzega, Tabora, Kigoma, Singida, Kasulu, Kibondo, Manyoni, Babati, Manyara, Karatu, Ngorongoro, Serengeti, Makuyuni, Arusha, Usariver, Dom city, Gairo, Kilosa. Musowero, Dumila, Dakawa, Turiani/Mtibwa, Madizini, Moro town, Matombo, Mzumbe, Mlali, Kimamba Kibaha zote, Dar km yoote na Udom&Ng'ong"ona. Kumbe nami nimekaa sehemu nyingi! Ngoja nianze kwenda kusini sasa, then nje.
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Zunguka kote lakini miji mizuri kuishi hapa TZ ni Moshi na Arusha!
 
Nimezunguka mikoa karibu yote kasoro Kigoma na Zanzibar....
Kwangu mbeya na mwanza palinivutia....
Mji.unaokua taratibu ni sumbawanga, tanga na ruvuma....
Mkoa wenye barabara hatari ni ruvuma kuanzia kuingia mpk ukanyage mbamba bay mpaka tunduru ni kona za hatari....
Hivi mpanda itakumbukwa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunafanana.. sujafika Zanzibar kwa maana ya kujua maeneo.. NIMEISHIA AIRPORT TENA NDANI YA NDEGE...
Mbeya palinivutia sana
 
Hamjajua tu wadogo zangu,,,,,,,mkoa Wa ajabu kuliko yote hapa bongo ni mbeya.....nilifika huko nikaishi kama miaka mi NNE.

Jamani ule mji ukiachana kabisa na pale mbeya mjini, yani kila sehemu panavutia kuishi na kila mji uliopo ndani ya ule mkoa umechangamka mpka nikawa nashangaa...

Mkoa wa mbeya ulinivutia sana kuliko mikoa yote niliotembea.......
Arusha na Moshi ni mikoa mizuri tu kimuonekano Wa juu juu na mandhari zake pale mijini lkn ukiingia ndani ndani hali zinatisha......na kusema ukweli ni mikoa ambayo ili uweze kuishi pale basi lazima uwe ni mtu Wa kipato kizuri sana.

Lakni Kule mbeya kwa wanyakyusa,wasafya, wanyiha wandali na wakinga ndugu zangu unaweza kuishi hata kama ni MTU Wa kuingiza Tsh 3000 tu kwa siku katika biashara zako.

Hali ya hewa ni nzuri na ina alternate..(Joto kiasi kwa kipindi flani na baridi ya mizuka kwa kipindi flani)

Kuhusu ardhi hilo ndo halina ubishi,,,,,,hata mazao karibu yote yanakubali kule Mbeya.

Mji umejengeka in some extent inaridhisha.

Shida ni moja tu mbeya.......

VIJANA WA KULE NI WAKOROFI SAAAAAAANAAAA YANI SAAANAAAA.........tena wote,,,,akuna cha mbeya mjini sjui tukuyu wala kyelaa au mbozi tunduma....yani ukorofi ni kama jadi yao na ma overconfidence ya ajabu ajabu...

Na lugha zao za asili wanaziongea kinoma kuliko kawaida.......!!!!

Mi ni mzaliwa Wa Tanga Handeni.
Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshukuru Mungu nimetembea kiasi chake hii Nchi Yetu.

Maeneo mengi yanakaribia kufanana.

Ila Kati ya hiyo hakuna palipozidi nyumbani Arusha. Napapenda sana kwetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom