Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Ambao tumezunguka Tanzania yote!

Just Distinctions

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2016
Posts
3,322
Reaction score
6,998
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Songwe,Tunduma pazuri sana,hari ya mvua na baridi,mwaka mzima unapiga pull over tu,nilipapenda sana,tatizo ni huduma ya maji,maji ya visima yalinisumbua sana.
Kahama,Geita pazuri kwa biashara,na ni mji unaokuwa kwa kasi sana.
Masasi,biashara ya mbao,na madini,wenyeji hawana makuu kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimezunguka mikoa karibu yote kasoro Kigoma na Zanzibar....
Kwangu mbeya na mwanza palinivutia....
Mji.unaokua taratibu ni sumbawanga, tanga na ruvuma....
Mkoa wenye barabara hatari ni ruvuma kuanzia kuingia mpk ukanyage mbamba bay mpaka tunduru ni kona za hatari....
Hivi mpanda itakumbukwa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ruvuma kwenda Njombe pia kilima kikali chief na kona za hataree ...karibu sana kigoma Ujiji ni parefu kwa Bus ila pako vizuriii sana
 
Mkuu masasi kuna madini..?
Songwe,Tunduma pazuri sana,hari ya mvua na baridi,mwaka mzima unapiga pull over tu,nilipapenda sana,tatizo ni huduma ya maji,maji ya visima yalinisumbua sana.
Kahama,Geita pazuri kwa biashara,na ni mji unaokuwa kwa kasi sana.
Masasi,biashara ya mbao,na madini,wenyeji hawana makuu kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimezunguka mikoa karibu yote kasoro Kigoma na Zanzibar....
Kwangu mbeya na mwanza palinivutia....
Mji.unaokua taratibu ni sumbawanga, tanga na ruvuma....
Mkoa wenye barabara hatari ni ruvuma kuanzia kuingia mpk ukanyage mbamba bay mpaka tunduru ni kona za hatari....
Hivi mpanda itakumbukwa lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpanda kuna fursa nyingi sana na hata kilimo kiko vizuri ila natumai serikali iliyopo italitupia macho hilo, umefika wakati sasa kwa kila wilaya iunganishwe na wilaya nyingine kwa barabara ya lami na mawasiliano mengine nchi nzima. Hatua hii itachochea sana maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Songwe,Tunduma pazuri sana,hari ya mvua na baridi,mwaka mzima unapiga pull over tu,nilipapenda sana,tatizo ni huduma ya maji,maji ya visima yalinisumbua sana.
Kahama,Geita pazuri kwa biashara,na ni mji unaokuwa kwa kasi sana.
Masasi,biashara ya mbao,na madini,wenyeji hawana makuu kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hakika,Maji ni tatizo kubwa kwenye sehemu nyingi nilizotembelea. serikali na sekta binafsi wote kwa pamoja tunapaswa kuwekeza kwenye hii sekta kwa mustakabali mzuri wa taifa letu. Kuna baadhi ya sehemu unakuta maji ni chumvi tupu kila ukichimba kisima ni chumvi yaani ni shida, maji yasiyo na chumvi ni bonge la deal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima, ni mara chache sana kutokea kupata fursa ya kuzunguka nchi yako, hasa kwa wale ambao nchi zao ni kubwa kidogo na Pia hawana shughuli za kuwafanya wazunguke kama wanamuziki, meneja wa kampeni au wakimbiza mwenge.

Mimi kama walivyo wachache katika wengi nimepata bahati ya kuzunguka nchi nzima na kuishi baadhi ya sehemu ukiacha zile ambazo nilizaliwa, nikakulia, au kusoma.

Huu uzi ni maalum kwa ajili hiyo tuelezee katika sehemu zote ulizozunguka ni wapi palikuvutia sana mpaka ukatamani hata kuishi

Nikianza na mimi, moja ya sehemu hizo ni karagwe huko kagera kwanza hali ya hewa ni nzuri sana afu ile milima ukiachilia mbali wachumba na misosi nilitokea kupaelewa sana.

Sehemu ya pili ni Iringa, aisee iringa ni poa sana kwanza hata mji jinsi ulivyokaa ni kivutio tosha, ni mji ambao umekua wenyewe na unapendeza tofauti na dodoma ambapo serikali inajaribu kila leo kupabeba lakini hapabebeki. Nahisi Iringa ingekuwaga makao makuu ya nchi ule mji ungekuwa mbali sana.

Sehemu ya tatu, ni lushoto dah hii hata sitaki kuelezea ila natumai mliowahi kufika mnapajua fika lushoto ni mji mzuri yaani mtu unaweza kutamani utafute kitalu afu ujenge mjengo na uishi.

Hizi ni sehemu chache sana hapa Tanzania je we umewahi kutamani kuishi wapi? Share nasi ili tufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
HAPO Kagera ni wilaya zote kuanzia
Ngara,Muleba,biharamulo,Bk Rural and Urban na hata karagwe maaeno ya Nyakahanga,Mulushaka etc pote nilichafua.
Enzi nasaka Kahawa na ndizi nazisafirisha ki Magendo..
Nilikuwa sipendi ile pombe yao ya Ndizi.

Tukija Njombe Kule town maeneo ya kuazia Ramadhani,hagafilo,Chaugingi,Kibena,Uzunguni,Tanwat pote Nilikanyaga WAKATI tunasaka madalali wa mashamba ya mbao.
kule lupembe Na matembwe karibu na Shule ya manyunyu niliruka Sana na pipoz za Kule daah Enzi tunaenda lupembe kusaka maparachichi na kuyasafirisha nje.
Tumelangua Sana mpaka tukapata mashamba ya maparachichi kule.

Kufika maeneo ya makambako tulikuwa tunafanya udalali,na kuuza vitu coz makambako ilikuwa Ni centre ya wafanyabiashara karibu wa kusini.

Tukija Iringa daah.
Sitopasahau kule pagawa na maeneo ya mtandika lukosi,
maisha ya kulima vitunguu yalikuwa magumu na full ushirikina.

hapo Morogoro,Dar,Tanga na Pwani sisemi maana naendaga ZAIDI navyokwenda msalani.

Tour Ambayo Nili enjoy Ni ile niliyozunguka mikoa ya Kusini
Kule pesa Ngumu lakini people's za Kule bado hazijajanjaruka ilikuwa Ni full kuwalaghai.

mkoa wa Kigoma sikuupendelea Sana
coz ya wingi wa wakimbizi na muingiliano wa warundi,wacongo na waha
hahahaha utaomba pooo

Wewe mleta maada umezunguka mikoa less than 5 .Kati ya mikoa 30?!

bado SANAA

Kwa Sasa naisaka njia ya Tunduma kutokea Momba




Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom