Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema usafi uliopangwa kufanyika hautaathiri maandamano yaliyopangwa kufanywa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Januari 24 iwapo watakuwa na kibali cha kufanya hivyo.
Chalamila ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Januari 22, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema Jeshi la Polisi ndilo lenye kutoa kibali cha maandamano.