Chalamila: Sina taarifa za maandamano, atakayejifanya takataka naye atabebwa siku hiyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema hana taarifa za maandamano ya Chadema yaliyotangazwa kufanyika Januari 24, mwaka huu akisema anachojua siku hiyo ni ya kufanya usafi.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 15, 2024 katika mkutano wake na watendaji wa Serikali kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Chalamila amesema watu wanahusisha shughuli ya usafiri aliyoitangaza na maandamano ya Chadema ambayo yeye anadai hana taarifa nayo.

Hata hivyo, amesema wakati baadhi ya watu wakihusisha tukio hilo la kufanya usafi na maadamano ya Chadema, yeye hana taarifa hizo kwa kuwa anayepaswa kuzitoa ni Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

"Mimi sina taarifa za maandamano na pia shughuli za watu wengine haziwezi kusimamisha shughuli za Serikali, ninachojua siku hizo ni kampeni kabambe ya kufanya usafi," amesema Chalamila.

Aidha, kuelekea Janauri 23 na 24 mwaka huu ambayo ilitangazwa kuwa siku ya usafi utakaohusisha vyombo vya ulizi, Chalamila, amewaonya wananchi wabishi kutoa fedha kwa ajili ya kuzoa taka.

Amesema siku hiyo ni ya usafi kabambe, lakini ana taarifa za baadhi ya wananchi kugomea kutoa tozo ya taka, hivyo kuwaonya kuwa siku hiyo ya usafi watachukuliwa hatua.

Kadhalika Chalamila amesema kuna haja ya kutengenezwa sheria ndogondogo za kusimamia utekelezaji wa utoaji fedha ya kuzoa taka ili atakayekaidi achukuliwe hatua mara moja.

"Kuzolewa taka sio jambo la hiari bali ni la lazima kwa kuwa umezizalisha mwenyewe na zisipotolewa zitaleta magonjwa," amesema Chalamila.

Katika hatua nyingine, ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kutoa vifaa vya kufanya usafi siku hiyo ya Januari 23 na 24 huku akitangaza kila wiki usafi utakuwa ukifanyika.

Amesema Januari 20 anategemea kuanza kugawa vifaa vya usafi katika vyombo vya dola.

Mwananchi
 
Kila CHADEMA wakitangaza maandamano ndo wanakumbuka kufanya usafi sio? Ila naamini ipo siku hata wa baada ya miaka 50 wajukuu zetu wataskia haya mambo watakua wanashangaa sana.... Watasema mababu zao tulikua wapuuzi sana kwa kukubali kutawaliwa mara ya pili hata baada ya kupewa uhuru
 
images (3).jpeg
wagwadu gwadu wakifanya usafi.

images (2).jpeg
 
Kila chadema wakitangaza maandamano ndo wanakumbuka kufanya usafi sio? Ila naamini ipo siku hata wa baada ya miaka 50 wajukuu zetu wataskia haya mambo watakua wanashangaa sana.... Watasema mababu zao tulikua wapuuzi sana kwa kukubali kutawaliwa mara ya pili hata baada ya kupewa uhuru
Watoto wa Palestina ndio kiboko. Mizinga ya Isreal wanaizuia kwa mikono. Wengine wakisikia sauti ya fisi mwituni wanaficha mvunguni
 
Wewe ndo unatawaliwa, kufanya usafi ni kutawaliwa?
Umesikia mkuu wa mkoa kakataza maandamano?
Wewe fanya maandamano yako acha wanaofanya usafi wafanye.
Kila chadema wakitangaza maandamano ndo wanakumbuka kufanya usafi sio? Ila naamini ipo siku hata wa baada ya miaka 50 wajukuu zetu wataskia haya mambo watakua wanashangaa sana.... Watasema mababu zao tulikua wapuuzi sana kwa kukubali kutawaliwa mara ya pili hata baada ya kupewa uhuru
 
Ile misemo ya mwalimu wangu aliyokuwa anatuambia mara kwa mara kuiweka kichwani; ukiwemo huu wa a fool will remain fool whether he goes to school or not, na ule wa bora ukose mali, upate akili! hakika mpaka leo bado inaishi kichwani mwangu.
 
Wewe ndo unatawaliwa, kufanya usafi ni kutawaliwa?
Umesikia mkuu wa mkoa kakataza maandamano?
Wewe fanya maandamano yako acha wanaofanya usafi wafanye.

Usafi gani hapo?. Acheni unafiki. Yani mnasubiri CHADEMA itaje maandamano ndio mkumbuke usafi. Tena mnafanya hivyo kwa kulidharilisha jeshi.
 
Mhe. Chalamila kama maandamano ya amani yameruhusiwa na Katiba nashauri waache waandamane kwa amani. Kuwavuruga kutaleta uvunjifu wa amani na lawama zote zitaelekezwa kwa Serikali ya CCM na baadaye dunia nzima kuilaumu Serikali ya Tanzania.
 
Kila CHADEMA wakitangaza maandamano ndo wanakumbuka kufanya usafi sio? Ila naamini ipo siku hata wa baada ya miaka 50 wajukuu zetu wataskia haya mambo watakua wanashangaa sana.... Watasema mababu zao tulikua wapuuzi sana kwa kukubali kutawaliwa mara ya pili hata baada ya kupewa uhuru
Nakazia
 
Back
Top Bottom