12 February 2024
TASK FORCE / KIKOSI KAZI CHINI YA MKUU WA MKOA, CHAKAMATA WATU KADHAA MKOA WA DAR ES SALAAM
Hayo yasemwa na mkuu wa mkoa wa DSM alipokuwa katika operesheni maalum
View: https://m.youtube.com/watch?v=oHAwL1r-kfw
Mkuu wa mkoa ameyasema mbele ya mkuu wa wilaya ya kinondoni mkoani Dar es Salaam Mhe. Saad Mtambule na maofisa wa task force kufuatia hali aliyosema RC Albert Chalamila inahitaji aunde na kukiwezesha zaidi kikosi kazi / task force.
Sasa task force itajumuisha Polisi, na vikosi vingine siri kwa kuwa inaonesha kuna watu ndani ya vyombo vya umma wanahusika na magendo
RC Albert Chalamila asema atafurahi silaha atazongeza zikizaa matunda kwa kuwa dola haiwezi kuchezewa, na silaha zikitumika watu wasilaumu wala kupiga kelele.
Ukanda wa bahari wa kuanzia kusini kwa mkoa wa DSM Pemba Mnazi hadi Bunju mpakani na Bagamoyo mkoa wa Pwani ni maeneo yanayotumika kuingiza bidhaa za magendo toka Zanzibar.
Na hili pia ni tishio la usalama, maana mbali ya magendo pia silaha, nyaraka za kichochezi, 'hela chafu' n.k zinaweza kuingizwa kwa magendo kipindi hiki tukielekea uchaguzi zikitoka Zanzibar, RC Albert Chalamila aonya.
- RC Chalamila atangaza Operesheni kali kuendelea maeneo yote ambayo bidhaa hizo hupitishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 11, 2024 ametangaza kuendelea kwa Operesheni kali ya kudhibiti upitishwaji holela wa bidhaa mbalimbali za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo amesema yoyote atakaye kamatwa adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
RC Chalamila amebainisha bidhaa za magendo zilizokamatwa ni mifuko ya sukari zaidi ya 100, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya 700 pamoja watuhumiwa zaidi ya 7 ambapo ameagiza watuhumiwa wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Aidha RC Chalamila amesema bidhaa hizo zilizokamatwa zimetoka upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutumia mashua " Kushamiri kwa uingizaji wa bidhaa za magendo ni kulikosesha Taifa mapato lakini pia ni hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa bidhaa hizo zinakuwa hazija pimwa ubora" Alisisitiza RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila amesema lazima tulinde kama tulivyo kula kiapo hatuwezi kuruhusu magendo katika Mkoa huu tuko imara sana kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii na amani ya Taifa hili
Ifahamike kuwa bidhaa hizo za magendo zimekamatwa usiku wa kuamkia jana Februari 10 kupitia kikosi kazi cha kudhibiti mtandao mzima wa upitishwaji wa bidhaa za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi
Source : https://dsm.go.tz/new/watuhumiwa-zaidi-ya-7-wakamatwa-dar

Watuhumiwa Zaidi ya 7 Wakamatwa Dar
Posted On: February 11th, 2024- RC Chalamila atangaza Operesheni kali kuendelea maeneo yote ambayo bidhaa hizo hupitishwa.