Ajira za walimu: Serikali kuajiri kwa kuangalia kigezo Cha umri wa mwombaji na sio mwaka wa kuhitimu chuo

ilikua kipindi hicho unaambiwa kasomee ualimu ajira uhakika ,ila saivi imekua tofauti
 
True
 
Kama ajira limekuwa kaa la moto huko serikalini hadi watu wanasagiana kunguni kuhusu umri, kwa nini wale ambao wameshapiga miaka 15 wasipwe nafasi ya kustaafu wawapishe wengine badala ya kukomaa mtu hadi afikishe miaka 60.....wakitoa hiyo option watu wataanza kustaafu wakiwa na miaka 40 hadi 45 kwa wale wanaoanza kazi kati ya umri wa miaka 25 na 30..........hawa watakaostaafu mapema wanaweza kujiajiri kwenye taaluma zao au kwenye maeneo mengine na kutoa ajira zaidi.....

Serikali iliangalie hili, kuna watu wanafanya kazi serikalini hadi wanachoka ila wanabanwa na kanuni na kushindwa kutoka kwenda kufanya ishu zao au kuhamia sekta binfasi. Wakati mwingine mtu anatathmini malengo aliyofikia na mahusiano yake kazini anaona anahitaji kubadili kazi lakini serikalini mtu unakuwa unabanwa sana na kanuni...........​
 
Kuna Watu wamemaliza mfano, mtu kasoma bachelor Biolojia Au mathematics amekaa mtaani miaka 7 tuseme amesoma 2012 baadae akaona hapati kazi akaenda kusoma postgraduate ya ualimu wa hayo masomo, let say mwaka jana 2021.
Bado kwenye kuajir wanasema huyu mtu ni muhitimu wa karibuni akati hata umri utakuta yupo kwenye 37 yrs huko.
 
Hili naona watu hawalioni. Si kila aliyechelewa kumaliza alikuwa anapiga mishe mtaani
Ni kweli yaani kupata kazi ya ualimu siku hizi ni bahati
 
Kumbe Samia katangaza nafasi za ajira kwa walimu elfu kumi,mbona sukuma gang hawalisemi hili, Ngosha hajawai kuajiri mpk mauti yanamfika,halafu leo anasimama mtu kama Mudawote amevimbilwa futari yake ya mafenesi anakuambia Samia hafai! Pumbavu kabisa!!
 
Aiseh!sijui tusomeshe watoto wetu kitu GANI!!!?kama ajira hamna halafu Elimu yenyewe mbovu haiwezi kumfanya mtu kujiajiri!!Mbona shida kubwa Sana!!
 
kidereko kwanza lugha za matusi hazifai. Hakuna aliyesema Mama Samia hafai, Mama kwa utendaji wa kazi hakuna shaka ni mtendaji mzuri. Kinachomharibia ni yeye na uhusika wa kifo cha Dkt Magufuli na hii inatokana na kauli zake tata za kumsema hayati vitu ambavyo walikuwa viongozi wote hata kama alitengwa alipaswa aheshimu kiapo chake. Mama Samia ni kiongozi mwenye exposure na uelewa mpana wa mambo ila kinachowachanganya watanzania ni kauli zake tata, kukumbatia watu ambao kabisa wana kasoro au mapungufu. Hivi kwa mfano angeteua timu yake ambayo haifungamani na Dkt Magufuli au Dkt Kikwete nani angemdharau? Sasa hivi kauli zake zote hasa za kumkejeli Hayati Dkt Magufuli zinatafasiriwa huku mitaani kama vile alihusika, na kibaya zaidi Mama alikuwa anapendwa sana tena sana na watanzania wanyonge, yaani alikuwa Mama kweli. Ila kwa sasa unakuta rais kabisa na mamlaka yake anatamka hadharani vitu vitapanda bei, mara tozo etc, kwa nini asijifunze kwa Dkt Magufuli ambaye mpaka sasa watanzania wanamlilia kila kauli ya kumsema ikitamkwa. Mama muambie kuwa kuna mstari mwembamba sana kati ya yeye kushinda uchaguzi 2025 na upendo wa watanzania, chuki iliyopo ni kubwa sana juu ya kifo cha Dkt Magufuli.
 
Pole Sana,kubarini tu magufuli ashakufa hatorudi Tena bibie, sorry Kama nimekukwaza best,

Muunge mkono Rais wako, huna namna zakufanya kumzuia Samia asiendelee Tena 2025, wenzio wamejipanga zaidi na zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…