Brightly
JF-Expert Member
- Apr 28, 2022
- 261
- 353
Habarii wanajf, hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya taasisi za umma zikianza kuajiri zenyewe badala ya utumishi ikiwa ni miezii kadhaa tangia Rais wetu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan alipozipa taasisi za umma mamlaka ya kujiendesha zenyewe kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na kuajiri bila kupitia utumishi.
Kitendo Cha serikali kuruhusu taasisi za umma kuajiri zenyewe ni kujitengenezea bomu ambalo litakuja kulipuka huko mbeleni.
Tunafahamu kuwa tatizo la ajira katika nchi hii ni kubwa Sana,ajira zinazotolewa na serikali ni chache Sana ukilinganisha na wanaohitimu kila mwaka licha ya ajira hizo chache Secretariat ya ajira (Utumishi) imesahaulisha wahitimu wengi kuhusu tatizo la ajira na imewajengea imanii kuwa ukijiandaa vizurii na ukawa competent unaweza kupata ajira serikalini Muda wowote bila kujuana na mtu yeyote.
Utumishi wamekuwa wakiendesha usailii kwa haki kuanzia namna ya kutangaza nafasi za kazi,kuita kwenye usaili,wanavyotunga mitihani yao hadi wanavyofanyisha watu usailii ni kwa hakii kwa asilimia zaidi ya 99% na hata ukikosa unajua kabisa siku yangu haijafika ipo siku yangu na unaona kabsaa Kuna haki imetendekaa.
Taasisi za umma kuajiri zenyewe ni kukaribisha Tena rushwa, ukabila, ukanda, udini, na unamjua nani? Hayo tunayashuhudia kupitia hizii ajira zinazotangazwa bila kupitia utumishi na hii inafanya wahitimu wengi kujenga chuki na serikali na kuona kuwa hawana haki ya kuajiriwa serikalini.
Tunamuomba Rais wetu mama yetu Dr. Samaia Suluhu Hassan ajira zote za serikali ziwe za kujitolea,za mikataba au za kudumu zipitie utumishi ili tushindane kwenye uwanja wa haki na hii italeta ufanisii hata katika kazi kwa sababu tutapata watu ambao ni competent ambao watafanya kazi kwa uweledi.