Mtwara wameanza kujitambua.. Mtwara haikuwahi kuwa na Mbunge wa upinzani tangia 1995, Mtwara haikuwahi kuachia Halmashauri zake zitawaliwe na Upinzani. Lakini mwaka huu katika majimbo 9, Ukawa wamechukua matatu pamoja na Halmashauri zake, Imechukua Halmashauri ya Newala Mjini hapo MKUCHIKA alilazimisha kushinda ila kiuhalisia alishindwa, CCM imeshinda kiuhalali Majimbo 3, Jimbo moja walilinunua mapema na Jimbo moja litaenda UKAWA 100%.. So kwa MTWARA ngoma itakuwa Ukawa 4 CCM 5 and It's not a bad start...
Kwa kura za URAIS ni dhahiri wameiba kupita maelezo, huko MAGUFULI jimbo alilomzidi LOWASSA kihalali ni LULINDI, NEWALA VIJIJINI na MTWARA VIJIJINI Pekee ila kwingine kote LOWASSA alimkimbiza MAGUFULI kwa mbali sana.. Nadhani kosa pekee la UKAWA huko ni kutoweka wasimamizi imara wa kura za Urais na ucheleweshaji wa matokeo ya Wabunge ambao uliwapa mwanya wa CCM kuchakachua kura za Rais..
Strategy ambayo CCM wanaitumia mwaka huu ni kuchelewesha matokeo ya Wabunge katika majimbo mengi nchini ili wabunge na wananchi wakiwa busy kuhesabu na kudai matokeo wao ndio wanapata mwanya wa kuchakachua kura za Rais maana wakati huo Mbunge na UKAWA wote kwa jumla wanakuwa wanatoa macho kwenye kura za Mbunge wao na kusahau za Rais.. Haiwezekani sehemu ambazo UKAWA wamechukua Jimbo, wamechukua 75% ya kata zote alafu MAGUFULI amkimbize LOWASSA kwa mbali.. Haya mambo ya Uchaguzi ni Ujinga na kupotezeana muda tu