Watu wa Mwanza, Arusha na Mbeya wanafuata nini Dar?

Watu wa Mwanza, Arusha na Mbeya wanafuata nini Dar?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
1,773
Reaction score
3,878
Hivi Tanzania haiwezi kujenga majiji mengine vizuri yakawa makubwa na maarufu kama Dar es salaam? Inakuwaje kila m Tanzania anataka kuishi Dar? Hivi Dar Peke yake ndio kuna maisha? Au wanazuzuliwa na umaarufu wa jiji la Dar? Watu kutoka mikoa kama Lindi, Mtwara, Mo to go to etc wakija Dar kutafuta maisha inaweza kuelezeka, lakini how comes watu wa majiji makubwa na yenye fursa nyingi kama vile Mwanza, Arusha na Mbeya nao eti wanakuja Dar kutafuta maisha?

Hivi Tanzania haiwezi kuwa kama South yenye JOHANNESBURG, PRETORIA, KZN ( DURBAN), CAPE TOWN etc. Majiji makubwa yenye umaarufu na fursa sawa? Inapaswa kuwa hivyo.. Watu wa Mwanza wanapaswa kuijenga Mwanza yao. Mwanza iwe ndio Dar es salaam ya kanda ya ziwa. Kule nyanda za juu kusini iwe Mbeya, kaskazini iwe Arusha na kusini iwe Mtwara..

Najisikiaga vibaya sana kuona watu wa Mwanza , Arusha na Mbeya wanakuja Dar kubanana huku wakati mikoa wana go toka ni mikubwa na mizuri tu. . Hasa watu wa Mwanza wanakosa kabisa uzalendo na mkoa wao. Mtoto wa Arusha anaweza kuvaa T. shirt imeandikwa " Chuga Boy" lakini mtoto wa Mwanza anaweza asivae T. shirt iliyo andikwa " Rock City Boy ". mi nafikiri kwa sababu Mwanza inahusishwa na wasukuma na usukuma unahusishwa na ushamba ndio maana watu wa Mwanza wanaona noma kuipigania Mwanza yao hadharani Ila Mwanza ni bonge Moja la place. Yani ni kama kanchi vile. Ni sehemu Moja tamu sana Mwanza hasa ukiwa na hela..

Ushauri: Kinacho wafanya watu wa mwanza, arusha na mbeya kukimbilia dar es salaam ni tatizo la kisaikolojia ambalo limekuwa motivated na media.. Media za tanzania zinaripoti sana habari za dar es salaam. Ukienda tiktok na instagram huko video zinazo trend ni za watoto wa dar. Lakini watu wa mwanza mbeya na arusha wakiwekeza kwenye media kupromote majiji yao basi after ten or twenty years hiyo hali ya kuitukuza dar itaondoka , population itapungua. Watu wengi wataenda mwanza, mbeya, arusha, mtwara, tanga etc kutafuta maisha / kuwekeza na population dar itapungua
 
Arusha imejaa matukio mara mama kabakwa hujageuka aua mtoto kisa kuonja mchicha.... Sijui baba abaka wazungu hujapumua sjui teleza avamia nyumba za watu nibaki dar kwa mtogole hapa
 
Dar nayo ya hovyo tu
Jiji lote joto,jiji linanuka,wakazi wake hawaogi hawapigi mswaki full kunuka,foleni,ushoga,mvua ikinyesha shida,kuoneana wivu,vyakula vya ajabu nk.
Nikiona mtu ametoka mwanza,mbeya,arusha anakuja dar kutafuta maisha namshangaa sana.
 
Dar nayo ya hovyo tu
Jiji lote joto,jiji linanuka,wakazi wake hawaogi hawapigi mswaki full kunuka,foleni,ushoga,mvua ikinyesha shida,kuoneana wivu,vyakula vya ajabu nk.
Nikiona mtu ametoka mwanza,mbeya,arusha anakuja dar kutafuta maisha namshangaa sana.
Plus mijitu inathamini chakula kuliko utu..mji wa kisenge
 
Back
Top Bottom