tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,778
- 29,228
Wahenga mtakubaliana na mimi 100% kwamba miaka ya nyuma mvua zilizokuwa zikinyesha Dar es salaam hazikuambatana na radi hata kidogo. Tulizoea kusikia matukio ya radi hasa huko Kigoma, Shinyanga, Tabora na mikoa mingine ambako matukio ya watu kuuliwa na radi yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara. Mvua za Dar es Salaam na Pwani zilikuwa za kumbembeleza mtoto alale.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, miaka ya karibuni kumekuwa na radi nyingi sana mikoa ya pwani hasa wakati huu wa mvua za masika. Kwa mfano siku ya leo (18.3.2026) wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo Jiji la Dar es Salaam wameuliwa na radi wakati wakicheza shuleni kwao. Hili limenilazimu, kama mtaalamu wa hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi, kutoa elimu kuhusu chanzo cha kuongezeka kwa matukio ya radi ukanda wa Pwani na Dar tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Radi na ngurumo zinazoambatana na mvua za hivi karibuni mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zinasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa unyevu angani wakati wa msimu wa masika. Mvua hizi mara nyingi huambatana na radi kali. Kwa ufupi, chanzo cha kuongezeka kwa radi katika ukanda huu ni:
1. Kuongezeka joto na unyevu angani, hali ambayo husababisha radi na ngurumo.
2. Mabadiliko ya hali ya hewa duniani yamefanya mifumo ya mvua kuwa kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kuleta ngurumo, kitu ambacho kilikuwa nadra hapo awali.
Namna ya kuepuka kupigwa na radi ni kutokaa chini ya miti mirefu au nguzo za umeme na kuepuka kutembea peku ndani ya maji wakati mvua inaendelea kunyesha. Ni afadhali usimame kwenye uwanja mweupe unyeshewe ulowe kisha utakauka badala ya kujikinga mvua chini ya miti na nguzo ndefu, huku ukihatarisha maisha yako bila sababu ya msingi.
Nawasilisha.