Abdulrahman Kinana: Chaguzi za 2019 na 2020 zilileta hofu, Mwaka 2024 na 2025 zitakuwa za Huru na Haki

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
GH5daOkWcAA4jSj.jpg

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"

"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"

"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Chanzo: EATV
 
Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli...
Kinana kwani Huo mwaka CCM walikuwa madarakani au walikuwa chadema? Hivi hawa waliosababisha hofu wapo madarakani au hawapo?
 
View attachment 2925116

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"

"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"

"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa
Ona huyu?😂😂
 
Aache maneno matupu mbona amegomea Tume Huru na Katiba Mpya?
 
Sasa huu uchaguzi wa hisani ya Rais ndio hatutaki.
Tuna hitaji katiba itafsiri uchaguzi sio ati Rais ame amua uwe huru!!! Hii ni akili au matope??
 
View attachment 2925116

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"

"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"

"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Chanzo: EATV
Kuna haja ya kupimwa afya kila wiki si mwezi ukialikwa mkutano wa upinzani unawahutubia kiupinzani aah ahahaha...!
 
JamiiForums-787880945.jpeg
Abdulrahman Kinana ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , leo amenukuliwa kwenye Mkutano Mkuu wa ACT WAZALENDO akidai kwamba Uchaguzi Mkuu wa 2024 na Ule wa 2025 utakuwa huru na haki , tofauti na ule wa 2019/2020

Sasa kabla hata ya kuendelea tunataka kujua , hapa Kinana anaongea kama Nani ? Ni mkurugenzi wa Halmashauri ambaye kwenye Uchaguzi atabadilika na kuwa Msimamizi wa uchaguzi au anaongea kama Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ? Ikiwa kama kinana anataka uchaguzi huru na haki ilikuwaje akashiriki kuvunja Maridhiano ya Chadema , ambayo yalijaa mipango ya kisheria iliyolenga kuwa na uchaguzi huru na wa haki , bila kuteka na kuua wagombea wa vyama vingine ?

Kinana analenga kumdanganya nani ikiwa anazo tuhuma mbichi zenye ushahidi mwanana wa kuchepusha matokeo ya Uchaguzi mkuu 2015 ? , nani amesahau jambo hili ? mtu kama huyu anawezaje kuaminika leo kwa kauli tu huku akikataa katakata mapendekezo mazuri ya Chadema yaliyojaa haki tupu za uchaguzi ?
 
Back
Top Bottom