Ya uchaguzi wa 2019 na 2020 yamejirudia uchaguzi wa marudio wa madiwani. Tutarajie uchaguzi mbovu tena 2024 na 2025

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,035
Hakika nimeukumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2019 na 2020 jinsi Rais magyfuli, CCM tume ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo uvuruga uchaguzi ule mpaka wahusani wetu wa nje wakakata misaada na mikopo kutokana na uchaguzi kuwa wa vurugu na mateso makubwa kwa wanachama na wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na kupelekea kukamatwa kwa makosa ya kubambikiziwa.

Juzi umefanyika uchaguzi mdogo wa madiwani yaliyojili ni yale yale ya uchaguzi wa 2019 na 2020

Nikishauri chama kikuu cha upinzani CHADEMA kijitathimini kwa kina mbinu itakazotumia katika chaguzi za 2024 na 2025 kwani hakuna dalili za katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi kwani uwepo wake utabadilisha system nzima ya wizi wa kura, watendaji wa tume ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi kuwa sehemu ya CCM.

Kumekuwa na kuchelewesha kwa makusudi kwa uanzashaji mchakato wa katiba mpya na tume huru na badala yake viongozi wa CCM wanawahadaa wananchi kuwa hofu ya uchaguzi wa 2019 na 2020 hatajirudi tena na kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru na haki hebu jiulize kwa katiba ipi au tume ipi ya uchaguzi?

Ni ukweli usiopingika kuwa CCM inataka katiba hii na tume hii ya uchaguzi vitumike 2024 na 2025. Watanzania tujiandae kwa yale yale ya 2019 na 2020.
 
Back
Top Bottom