Andrew Nyerere: Komredi Abdulrahman Kinana ni mchochezi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200

Mtoto wa Nyerere aunga mkono maandamano nchi nzima

Andrew Nyerere mwanachama wa CCM akizungumza katika mkutano wa ndani wa CHADEMA , amkosoa makamu mwenyekiti wa CCM- Bara komredi Abdulrahman Kinana kwa kutoa maneno yakichochezi dhidi ya haki ya CHADEMA kuandamana.



Naye classmate wa komredi Kinana, Mzee Zonga Mafie waliyesoma naye shule na kukaa desk moja aliyepitia TANU youth league, CCM amekosoa mwenendo mpya wa utawala wa CCM kuua viwanda vilivyokuwa vinatoa maelfu ya ajira kwa vijana. Classmate asema CCM ya sasa haina uwezo wa kujenga mamia ya viwanda kama enzi za baba wa Andrew Nyerere yaani baba wa Taifa Mwl. J .K Nyerere

Komredi kanali mstaafu Abdulrahman O. Kinana wasifu CV wake unasema ambaye pia alipata kuwa spika wa bunge la zamani la Afrika ya mashariki EALA, Katibu Mkuu CCM, Makamu mwenyekiti CCM awamu ya Kikwete, waziri wa ulinzi wa serikali ya Tanzania, naibu waziri mambo ya nje, naibu waziri ulinzi, mbunge wa Arusha mjini kupitia CCM, Mjumbe wa Kigoda cha Mwl. Julius Nyerere.

1707351434255.png

Komredi Kinana jumapili juzi tarehe 4 February 2024 akiongea na makada wa CCM jijini Dar es Salaam alikosoa vikali haki ya CHADEMA kuandamana. Kinana alizungumza mengi ikiwamo :

*Achambua ubora wa sheria mpya ya uchaguzi, atoa rai kwa watanzania

*Awataka Chadema kuona nia njema ya Rais katika kuleta maendeleo

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhman Kinana, ameshauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini nia njema aliyonayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maridhiano na kuwatumikia Watanzania.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina ubora wa sheria ya uchaguzi ambayo imepitihswa na Bunge hivi karibuni, baada ya wadau mbalimbali nchini kutoa maoni yao ambapo amesisitiza sheria hiyo ni bora kuliko iliyopo sasa.

Kinana ameyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na wana CCM na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo mbali ya kutumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM na CHADEMA pamoja vyama vingine vya upinzani, alisema kuna mambo mengi mazuri yamefanyika.

Amesema mambo mazuzi yamefanikisha kupata mwafaka ingawa CHADEMA haitaki kueleza ukweli ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh.bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

"Kupitia maridhiano CHADEMA wamenufaika sana, kulikuwa na hoja 11 na zotw ni za kwao, CCM hatukuwa na hoja hata moja, na hoja zote zilikubaliwa ikiwemo ya kutaka ruzuku yao ya miaka mitatu ambayo walikuwa hawajaichukua.Wamechukua ruzuku ya Sh.bilioni 2.7 na baada ya hapo wamekaa kimya wala hawasemi kama wamepewa ruzuku yao na Rais Samia."

Faida nyingine ya maridhiano ni CHADEMA wafuasi wapatao 400 waliokuwa mahabusu kwasababu mbalimbali karibia wote wameachiwa kasoro kesi mbili ambazo hizo zinahitaji mlolongo wa kisheria, kesi moja iko Njombe inahusu tuhuma za mauaji na kesi nyingine iko Kibaha inahusu tuhuma za dawa za kulevya."Zimebaki kesi mbili tu ambazo hizo zinahitaji zaidi utaratibu wa kisheria zaidi."

Kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?

Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali.

“Sasa niwasihi ndugu zangu Watanzania, tujipange kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, tujipange kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025. Sheria hii ni nzuri, bora kuliko sheria yoyote iliyopo katika historia ya nchi yetu, inakidhi mahitaji na matakwa ya nchi na jumuiya ya madola, inakidhi mahitaji ya nchi za Umoja wa Afrika (AU), inakidhi vile vile mahitaji ya nchi za Kusini mwa Afrika ambao na sisi ni wanachama,” amesema.

Amefafanua hakuna tume ya miujiza zaidi itakayokuwepo, huku akifafanua kila jambo ambalo litafanyika lazima litakuwa na kasoro moja au mbili, na kuhoji kwani CHADEMA wao hawana kasoro?

“Wanazo, sasa nawaambia ninyi chama kikuu cha upinzani kuweni basi na ustahimilivu kidogo, uungwana na kusikiliza wenzenu na kuona nia njema iliyopo katika Chama Cha Mapinduzi, kwa na serikali yake,” amesisitiza.

Akifafanua zaidi Kinana amesema kuwa kushinda uchaguzi kunatokana na sera, mipango ya uchaguzi na kusikiliza watu, kwani unaweza kuwa na tume nzuri ya uchaguzi na matokeo yakawa ni ya hovyo, usiyoyataka.

Ametoa mfano wa moja ya nchi jirani ambayo walipigania sana kuwa na tume huru kwa miaka 20, wakaipata, lakini wamegombea mara nne hawakupata.

“Hawakuingia madarakani, wale waliotengeneza hiyo tume hawakupata, sasa wanasema Katiba hii haina maana waifute, wale walioingizwa na katiba baadae nao wakashindwa wanasema katiba hii haina maana. Kwa hiyo aliyeshinda anasema Katiba haina maana na aliyeshindwa naye anasema Katiba haina maana.

“Sasa kushinda uchaguzi sio Katiba tu, Nigeria baada ya wanajeshi kutoka baradakani walitengeneza Katiba mpya mwaka 1969 na kwa sehemu kubwa walienda kuchukua Katiba ya Marekani, tume ya uchaguzi ya Rais inateuliwa na Rais kwa kushauriana na baraza la ushauri.


“Baraza la ushauri ni nani? Rais ndio Mwenyekiti, makamu mwenyekiti ni makamu wa rais, wajumbe wengine marais wastaafu, hapo vipi? Kuna mtu anatoka nje ya mfumo?

“Hao ndio wanateua, mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume, uchaguzi unafanyika na watu wanakubali. Hapa tunatafuta malaika wa kuja kuongoza tume, kila utakachofanya unaambiwa kinakasoro, hivi mnavyoona yote tuliyokubali wanasema hamna kitu.

“Nimesikia wanaandaa maandamano Mwanza, Mbeya na Arusha na mimi nataka niwasaidie kutangaza kama watu wengine hamjasikia. Wanakwenda kueleza haya yaliyopitishwa na CCM na Bungeni hamna kitu.

“Tume si kila kitu, Namibia kamati inatengenezwa baada ya pale anayetua Rais, kuna nchi inaitwa Mauritius na hizi nchi zote ambazo nimezitaja ni za Jumuiya ya Madola, Rais anashauriana na watu wawili tu, anashauriana na waziri mkuu na kiongozi wa upinzani bungeni hakuna mtu mwingine,” amesisitiza.

“India wana mkurugenzi na wana makamishina. Nani anateua? Waziri Mkuu na Baraza lake la Mawaziri kwisha, yaani Rais Samia akae na baraza lake la mawaziri atengeneze orodha ateue, si moto utawaka hapa? Watasema tu maigizo.

“Sasa kuna shida hapa nchini kila unalofanya halina heri ndani yake, lakini vizuri haya mambo tukayaeleza maoni mengine yakatolewa unajua siku hizi kuna watu wanapita bila kupingwa lakini ni vizuri wanaopita bila kupingwa wakapigiwa kura ya ndio au hapana Bunge likasema sawa tumekubali.

“Wanauliza kwa nini? Wanasema kuna watu wengine wanafanya ujanjaujanja wa kupita bila kupingwa, hivyo wapigiwe kura tujue kama wanakubalika Bunge limesema sawa itapigwa kura ya ndio au hapana,” amefafanua.
Mwisho.

2020 4 June

UTAMADUNI WA KUJISAHIHISHA




Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana amejitokeza, kujisahihisha na kumuomba msamaha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.
 
Inabidi usikilize hotuba yote ya Kinana kupata picha ya raisi Samia. Hata wao anti-Magufuli uvumilivu wa huyu mama unawashangaza.

Anachosema huyo Andrew Nyerere ndio hiko hiko; alichoeleza Kinana CDM wanapendekeza raisi asiwe na madaraka yeyote kwenye katiba mpya. Sasa majukumu yake atayatekeleza kwa mamlaka gani. Unabaki unajiuliza hivi hawa watu ata hiyo maana ya katiba wanailewa.

Pamoja na kupewa demand hizo zisizo na kichwa wala miguu; wanamueleza hawa watu wameshindikana. ‘Bi-Tozo’ anawaambia msiwasuse endeleeni majadiliano nao; salaleh,

Ulezi wa huyu kwa nchi iliyojaa majizi serikalini hakuna shughuli yaani hata baadhi ya matakwa mengine ya CDM kwa maelezo ya Kinana yamezuiliwa na vyombo vya usalama kwenye Issue za katiba na kwenye mambo ya jinai mahakama na polisi; yaani wao mpaka mtu alieuwa, mwili upo na ushahidi upo wanadai kasingiziwa; mtu ana kesi ya madawa ya kulevya wanadai kasingiziwa.

Huruma wa huyu mama atuendi popote, yaani hata hiyo nafasi ya Makonda inaonekana ni kwa ajili ya uchaguzi ujao tu.

Ukisikiliza upande wa CDM wanavyolalamika na ukizikiliza upande wa CCM kupitia hotuba ya Kinana jinsi walivyo wasumbufu. Ndio utaelewa Samia ni mdekezaji mno ndio maana nchi inachezewa (wanamuangusha sana). Kuongoza hii nchi huruma unataka mipaka.
 
Abdulrahman Kinana akielezea legacy ya Mwl. Julius Nyeree akihutubia chuo kikuu cha Carleton University


View: https://m.youtube.com/watch?v=l2eEICpFjf4
Keynote address by comred Hon. Abdulrahman Kinana at Institute of African Studies One Day Conference at Carleton University: "The Legacies of Nyerere: Economies, Politics, and Solidarities in Tanzania and Beyond" (March 4, 2011)
 
Naye classmate wa komredi Abdulrahman Kinana, Mzee Zonga Mafie asimulia jinsi chama dola kongwe kilivyokwama katika sera ya viwanda vikubwa


View: https://m.youtube.com/watch?v=QTh6x1Fr5pc

Mzee Zonga Mafie alikuwa akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya Maandamano ya Amani leo Jumatatu Februari 5, 2024 kilichochoshirikisha BAVICHA kujiandaa kwa maandamano siku zijazo ..
 

Toka maktaba / Archive :​

30 January 2024​

Tanzania Ruling Party and 2023 Electoral Reforms bills​


1707385070935.png


DAR ES SALAAM --Tanzanian lawmakers launched a debate Tuesday on proposed electoral reforms despite the objections of the opposition and some civil society groups.

Thousands of people had joined a demonstration called by the main opposition Chadema party last week over the legislation, which its leader Freeman Mbowe says contains only "cosmetic" changes.

But the government of President Samia Suluhu Hassan insists the reforms will improve governance and democracy in the East African country of about 65 million people.

Next year Tanzania is scheduled to hold its first presidential election since the death of authoritarian leader John Magufuli in 2021 led to his deputy Hassan taking the helm.
1707385795864.png

File photo : H.E. President Samia Suluhu Hassan

"The president has the good intention of improving multiparty democracy in Tanzania through reconciliation and reforms," said Jenista Mhagama, a minister of state in the president's office who presented the bills before parliament on Tuesday.

"The electoral reforms we discuss today are the outcome of recommended changes by a taskforce formed by different political stakeholders in Tanzania," she added.

Last Wednesday's demonstration in the main city of Dar es Salaam was the biggest since the government lifted a ban on opposition political rallies a year ago.

Mbowe, who has spent time in prison under both leaders, said the bills being debated do not address concerns over the last election in 2020, which Magufuli won by a landslide despite opposition claims of fraud.

The Chadema party has been campaigning for constitutional reforms and greater independence for the electoral commission to be included in the legislation.

Criticism of the proposals has been directed in particular at a measure that would allow Hassan to directly appoint five of the 10 members of the electoral commission.

"Our opinions and those of the political stakeholders have been ignored," Chadema secretary general John Mnyika said Tuesday.

He said on X, formerly Twitter, that the debate is set to run only until February 2 according to the parliamentary schedule.

"The simple interpretation is that they (the bills) are going to be passed without initiating amendments to the constitution."

Parliament is dominated by the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party which has 364 out of the 392 seats.

Hassan has sought to reverse some of the more hardline policies of her predecessor Magufuli, whose strongman tendencies earned him the nickname "Bulldozer."

A ban on opposition gatherings was overturned in January 2023.

Shortly afterwards, one of Tanzania's most prominent opposition leaders, Tundu Lissu, returned to the country after having spent most of the previous five years in exile.
 
2020 4 June

UTAMADUNI WA KUJISAHIHISHA



Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana amejitokeza, kujisahihisha na kumuomba msamaha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli

9 February 2024

TUNDU LISSU AMVAA CDE. ABDULRAHMAN KINANA "ALISHUGHULIKIWA / KUNA MAMBO TUNAYAJUA WAJIHESHIMU" AANIKA YA RAIS SAMIA UBELIGIJI"



View: https://m.youtube.com/watch?v=8eafKPLr5D0
 
Inabidi usikilize hotuba yote ya Kinana kupata picha ya raisi Samia. Hata wao anti-Magufuli uvumilivu wa huyu mama unawashangaza.

Anachosema huyo Andrew Nyerere ndio hiko hiko; alichoeleza Kinana CDM wanapendekeza raisi asiwe na madaraka yeyote kwenye katiba mpya. Sasa majukumu yake atayatekeleza kwa mamlaka gani. Unabaki unajiuliza hivi hawa watu ata hiyo maana ya katiba wanailewa.

Pamoja na kupewa demand hizo zisizo na kichwa wala miguu; wanamueleza hawa watu wameshindikana. ‘Bi-Tozo’ anawaambia msiwasuse endeleeni majadiliano nao; salaleh,

Ulezi wa huyu kwa nchi iliyojaa majizi serikalini hakuna shughuli yaani hata baadhi ya matakwa mengine ya CDM kwa maelezo ya Kinana yamezuiliwa na vyombo vya usalama kwenye Issue za katiba na kwenye mambo ya jinai mahakama na polisi; yaani wao mpaka mtu alieuwa, mwili upo na ushahidi upo wanadai kasingiziwa; mtu ana kesi ya madawa ya kulevya wanadai kasingiziwa.

Huruma wa huyu mama atuendi popote, yaani hata hiyo nafasi ya Makonda inaonekana ni kwa ajili ya uchaguzi ujao tu.

Ukisikiliza upande wa CDM wanavyolalamika na ukizikiliza upande wa CCM kupitia hotuba ya Kinana jinsi walivyo wasumbufu. Ndio utaelewa Samia ni mdekezaji mno ndio maana nchi inachezewa (wanamuangusha sana). Kuongoza hii nchi huruma unataka mipaka.

Mwamba ngozi huvutia kwake. Hiyo nafasi ya urais kusimamia tume ya uchaguzi imekuwa ikitumika vibaya, na ushahidi uko wazi na sio uchaguzi mmoja, japo uchaguzi wa 2020 uliweka wazi madaraka ya urais kunajisi uchaguzi. Unataka watu wakubaliane na mabadaliko kadhaa kama wajinga as if hawajui Nini kinaendelea? Ni hivi hakuna wa kukubali tena muundo wa uchaguzi usio wa haki, kama unadhani ni hisani mambo hayo Bado mnaweza kufanya mtakavyo, lakini sio kuleta hadaa ili watu wakubali mje na story za Nia njema ya rais.
 
Back
Top Bottom