A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Mgonjwa wa rafiki yangu alikufa kwa kukosekana vifaa vya kumfanyia operesheni. Je, hiyo ni mgomo wa madaktari. Tuweke uwigo mpana wa kujadili hili suala. Hata madaktari wakiwa kazini wagonjwa wanakufa kwa kukosa huduma. Mbona watanzania tunapenda kuhalalisha shida ambazo si shida .... maana huduma duni kwenye mahospitali ni matokeo ya UFISADI. Mbona hatuwasemi hawa mafisadi na kuingia mtaani kama tunavyowasema madaktari!?
 
Jamani naona watu mmecharge kama mafahali wawili ndani ya zizi! Ni vizuri kuwa na tahadhari kumhusisha Rais na kutekwa kwa Dr. Yes uongozi wake una matatizo lakini kumhusisha na hili jambo tunakwenda mbali. Kikwete si mtu wa visasi vya namna hii. Ana njia nyingi tu kama angetaka za kumdhibiti Dr. na asingekuwa na haja ya kutumia njia ya aibu namna ile.

Mtu anayesababisha shida ya madaktari ni waziri mkuu. Ameshidwa kumshauri rais ipasavyo kwenye jambo hili.

Mkuu kwenyen red hapo nadhani humjui vizuri JK. hakuna raisi aliwahi kuwa na visasi kama tuliye naye leo.
 
wanagoma na mwisho wa mwezi wanaenda na ATM kudraw Bank fedha zetu walipa kodi huku wagonjwa wetu wanakufa hospitali. hii ni halali? kwanini waendelee kulipwa mwezi huu? kwanini serikali haigomi kuwalipa kwa kususa kwao? hawatendi haki hata kidogo.

Hivi jana mama ako alilala nyumbani best?
 
Pole kweli wewe, hivi unawezaje kumuhudumia mgonjwa mahututi wakati huohuo unamwambia kalete Groves,

kwa huko vijijini mama mzizi anaambiwa njoo na na mafuta ya taa ya kuchemshia maji, kuwasha taa, groves na maji yake.

hii kazi ni ngumu sana na ni hatari pia (naamini unanielewa )

Kwanini ulisomea udaktari? ungesomea usecretary ili uendelee kuwa smart na kazi isiyo na hatari,hivi watumishi wengine wa serikali wakigoma kama madaktari nchi itatawalika?,kwa yaliyotokea hilo ni onyo na somo kwa madaktari ili mthamini na utu wa wengine eti kalete gloves! kwani huduma ni za bure! si analipa mgonjwa kwanza siyo mgonjwa anayenunua walio karibu yake au manesi wanafanya kazi hiyo na siyo daktari,eti kazi ya muhimu sana hivi mnajua kazi za muhimu nyie?.hivi kuna madaktari wangapi huko vijijini? ni sawa na hakuna wote wapo mijini wananchi wanakufa kama kuku huko vijijini hamuwatembelei na hata akifurukuta kuja mjini nako Israeli anamfuta kisa mgomo!mnakula nchi tu mijini,iko siku mkihamishiwa vijijini mnagoma na kuishinikiza serikali eheee hivi nchi hii yakwenu peke yenu,natak kulia R.I.P Dr. Ulimboka kama wale ndugu zetu wanavyokufa kule vijijini kama kuku mwenye mdondo.
 
Nakubaliana na mtoa hoja na ni kweli tukitanguliza hisia zaidi katika kutafakari hili jambo ukweli tutabaatisha na si kuupata tulichokiitaji kwa ujumla wake.
 
Anaendelea vizuri nimechart na jamaa yangu lhrc kaniambia jamaa anarecover ingawa kasema lengo la watekaji ilikuwa ni kuua na walijua wameua!!!!!!!!!!!ngoja nimcheki tena baada ya mida .

asante yesu
 
Mkuu umenena maisha magumu ni kwa kila Mtanzania...kila taaluma ina umuhimu wake.Watanzania wote tuwalaani madaktari kwa kitendo chao cha kinyama

Tunamuombea Dr. Ullli afya yake iwe back to normal the soonest, niliwahi kuhuliza humu hivi madaktari hao wakiondolewa vitendea kazi vyote na madawa wakabaki na talaaluma zao vichwani tu - wanaweza kweli kutibu watu bila kuwa na nyenzo hizo? Ninacho taka kusema hapa ni kwamba wakumbuke kwamba kuna wataalamu walio hunda vitendea kazi sophiscated vinavyo walahisishia kazi zao, je wataalum hao nao wakija juu na kuwanyanganya zana zote Madaktari, kutatokea nini.

Taaluma zote duniani zinategemeana, haipendezi kikundi cha watalaam fulani kujiona wenyewe ni zaidi katika nchi hii; niliona wana JF wanawasema vibaya walimu eti hawajasoma, wanaforge vyeti, mambo chungu nzima na kejeli - kuna mtu yeyote duniani anaweza kudhalau walimu kweli? kwani madaktari walipataje vyeti vyao kama sio kupitia kwenye msururu wa WALIMU!!!

Nalisema hili kuwakumbusha kwamba UZALENDO na UTU ndio upewe kipa umbele kwanza, kama Serikali iliyo wasomesha bure imekubali wayamalize matatizo kwa majadiliano kwa nini amuiamini mkawa wavumilivu/watulivu - mimi najiuliza sana, hivi haya ni mambo ya mishahara tu na marupurupu au kuna kitu kingine cha ZIADA nyuma ya pazia - wakumbuke pia kwamba maisha magumu ni kwa kila MTANZANIA.
 
Kitu ambacho sielewi inakuwa je polisi wanapewa taarifa ya kwamba mtu katekwa harafu wao:

1. Waanaangalia mahabusu zao na kusema hakuna taarifa za mtu huyo?
2. Njoo kesho asubuhi?
 
Madaktari hawapo katika kutetea huduma za afya wangekuwa wanatetea kuboreshwa huduma wasingekuwa wanagoma kuacha watu wafe. Wao wapo ki maslahi binafsi!

Unajitahidi sana kupotosha mada zote, hata zile zenye kujieleza pasipo mashaka. Nafikiri ni mmoja wao mliopandikizwa ili kufanya kazi za upotoshaji. Nimekuona kwenye thread nyingi ukiwa unapotosha mambo ama kukebehi. Nakushauri hili si jukwaa linalostahili kwani hauleti impact yoyote kutokana na uharibifu unaojitahidi kuujenga.
 
Kwanini ulisomea udaktari? ungesomea usecretary ili uendelee kuwa smart na kazi isiyo na hatari,hivi watumishi wengine wa serikali wakigoma kama madaktari nchi itatawalika?,kwa yaliyotokea hilo ni onyo na somo kwa madaktari ili mthamini na utu wa wengine eti kalete gloves! kwani huduma ni za bure! si analipa mgonjwa kwanza siyo mgonjwa anayenunua walio karibu yake au manesi wanafanya kazi hiyo na siyo daktari,eti kazi ya muhimu sana hivi mnajua kazi za muhimu nyie?.hivi kuna madaktari wangapi huko vijijini? ni sawa na hakuna wote wapo mijini wananchi wanakufa kama kuku huko vijijini hamuwatembelei na hata akifurukuta kuja mjini nako Israeli anamfuta kisa mgomo!mnakula nchi tu mijini,iko siku mkihamishiwa vijijini mnagoma na kuishinikiza serikali eheee hivi nchi hii yakwenu peke yenu,natak kulia R.I.P Dr. Ulimboka kama wale ndugu zetu wanavyokufa kule vijijini kama kuku mwenye mdondo.
Duh ningekuwa nafikiria kama wewe hata 1/10000000000000000000000000000000, ningeomba israeli anichukue:sad:
 
Kama ni kweli Rais huyu dhaifu atakuwa anakosea sana,ni mapema mno kwake kufanya hivyo Hapo MMC pako hot sana,yote haya ni kutokana na kuwa na washauri dhaifu pia.anataka kujikosha halafu aseme atapelekwa india ili wakammalizie huko Ashindwe na alegee na adondoke chini akikanyaga maeneo ya muhimbili.
 
Huyo Dr Ulimboka siyo COMANDO,atakuwa ni mla rushwa (CORRUPT) sana na inavyoonekana anaweza kuwauza wenzake.Nasema hivyo kwa sababu ukiiangalia hii incidence unaona kuwa huyu Dr Ulimboka ana tamaa ya pesa na anaendesha mgomo kwa kushawishi wenzake ili anufaike binafsi.Nasema hivyo kwa sababu hebu fikiria kwa akili ya kawaida tu,wewe una ishu kubwa kama hiyo ya mgomo,halagu unaitwa na mtu usiyemjua ili mkafanye reconcilliation na wewe unaenda tena peke yako!!!!.Bila shaka ni reconcilliation kuhusu mgomo.Hapo naona kuwa anaweza kuitwa na watu asiowajua na yeye akaenda tena peke yake!!!!.Baada ya hapo anaweza kuwageuka wenzake.HAFAI KABISA ANASUMBULIWA NA TAMAA NA NJAA TU.
Umejenga hoja kwenye dhana za uongo. Kwanza dk ulimboka hakuwa peke yake. Pili, hakuna maelezo yoyote mahala popote ktwa alishawishiwa kwa pesa, tatu, hakuitwa na mtu yeyote, bali alikuwa na wenzake Leaders club wakipata kinywaji.
 
nyie mnaomtetea dr ulimboka hana akili wote kwa sababu serikali haiusiki hata kidogo kwa swala la kupigwa kwa dr,na kwa taarifa yenu aliyehusika na kitendo hiki ni wananchi wenye hasira kali ni baada ya kupotelewa na kufiwa kwa ndugu zao
wewe ungekuwa na akili kuleta ujumbe wa wale waliokutuma bor mara 100 ungesema serikali inahusika kuliko kusema wananchi, so unamuua anaekutibu kesho atakutibu nani? So madk na manesi waache kuhudumia wagonjwa wote kwa vile mnawaua, hiyo serikali yako itabaki madarakani? Hata hujui kuwatetea waliokutuma, hapa serikali hawatoki, sijui hata mnapataje hizi kazi ilihali mnashindwa kufikiri cha kusema kwa mambo madogo km haya
 
Back
Top Bottom