Matukio ni mengi bali
nitawasilisha machache. Tukio la kutelekezwa Dk Harrison Mwakyembe
alipopata ajali mkoani Iringa, Polisi Usalama barabarani walidaiwa
kususia kutoa msaada eti tu kwa kuwa amekuwa akitoa misimamo mikali kwa
Serikali hususani Kamati aliyoisamamia kuchunguza Richmond. Mwakyembe
huyo huyo polisi kushindwa kutoa taarifa kuhusiana na waraka
uliohusishwa na mauaji yaliyoelekezwa kwake akishirikishwa na baadhi ya
wanasiasa wenye misimamo chanya. Mheshimiwa Samueli Sitaa kutishiwa
kugongwa na gari aina ya Hammer. Dk Slaa kuwekewa vinasa sauti chumbani
kwake,. Mwandishi wa habara Jerry Murro, pamoja na Jeshi la polisi
kupeleka ushahidi wa kuokoteza, lakini bado Muroro aliwagalagaza. Sued
Kubenea kumwagiwa tindikali, matukio ni mengi, cha ajabu ni hawahawa
Usalama na Mkuu wao wamekuwa viherehere kujikosha kwa kutembelea
hospitalini. Kuweni makini hawa si Usalama, hawa ni wana Uhasama.
Watanzania muanze kujilinda wenyewe, hususani kufanya mazungumzo na watu
unaowatilia mashaka. Kuitikia simu ambazo una mashaka nazo hususani
zenye ushawishi wa aina flani flani. Ukiwa unapitia kipindi kiugumu
epuka mienendo ya usiku. Yanayotokea Somalia si kwamba wamekosa kwa
Mwenyezi Mungu. Dalili ya Mvua ni Mawingu
TUWE MAKINI.