siyo ulihifadhi anaitwa Abeid
wakuu hapa JF naomba tusifanye propaganda kama kweli tunachukizwa na kitendo cha serikali kufanya ufisadi wa kupindukia,kufuja mali za umma kwa kufuru,serikali kutokushughulikia mambo ya msingi na kusababisha migomo isiyoisha kwa muda mrefu,kutoka kwa wafanyakazi na wanafunzi na hatimae leo tuko kwenye mgomo unaogusa moja kwa moja uhai wa watanzania hasa wenye kipato cha kati na cha chini,ni vema basi tusikae tunaficha ficha mambo hapa.
NAOMBA TUWATAJE HADHARANI WALE WOTE WALIOHUSIKA KUMTEKA DR ULIMBOKA,HAKUNA SABABU YA KUFICHA WATAJENI WOTE TUWAJUE KWA UWAZI,HATA PICHA ZAO WEKENI HAPA TUWAJUE.
Kuficha ni sawa na kuutetea unyama huo uliofanywa na huenda ukawa endelevu kwa siku zijazo.watajeni,wekeni na picha zao tuwajue hawa wauaji,na hata kale kapolisi mlikokashika Mhimbili wekeni hapa picha yake.mtu mwenye taarifa sahihi za tukio zima alilofanyiwa dr Ulimboka naomba mtuwekee hapa,msiwafiche hawa,tuwaanike walishazoea kuuwa.
Niwakumbushe wale wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mpaka leo haijulikani nani aliwauwa na hii ni kutokana na tabia ya kuficha mambo.kwa mwenye taarifa nawaomba tuweke hadharani.