A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
"Ndugu zangu,

Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".

Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.


Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy wa LHRC
Katika taarifa ya habari mtu aliyekuwa akimtafuta mfululizo kwa siku tatu ni mtu wa Ikulu aitwaye kwa jina moja David na baadaye aliondoka kumfuata huyu David na baadaye akatekwa infront of him. Kwa mwenye akili anajua tu hii ni plan from somewhere

Mbona hili wala sio siri tena ... Jamaa alimpigia simu wakamalize maongezi LEADERS CLUB!!! Ulimboka akaondoka na Rafiki yake mmoja! Wakati wanongea na huyo Jamaa hakueelwana ...

Jamaa akapiga simu kwa hao wanjeshi walikuja kumburuza na kumchukua ... wakamuacha Rafiki wa ulimboka na huyo jamaa mwingine kwa kusema hatuwahitaji nyie tunamuhitaji Dr Ulimboka ....!

Rafiki wa Ulimboka ... Akapiga simu kwa waaharakati wa Haki za Binadamu ..Hellen Kijo Bisimba at al .. na usiku huo wakaanza kumtafuta na kuripoti vituoa mbalimbali vya Polisi ...lakini Kila kituo wakidai ... hamjui huyo mtu .... labda waje asubuni .... na subuhi? Wapata habari toka kituo cha polisi tegata .... kaokotwa mtu ....blabalahhhh!!

Source. Hellen Kijo Bisimba!!
 
Hii sasa kali na inatoa sura ya nchi ilivyo kwa sasa.

kwa nini hiyo simu ya huyo kijana askari isingechukuliwa na kufahamu alikuwa akiwasiliana na nani.

Hii ndiyo serikali ya ccm na haya ndio maisha bora kwa kila mwanchi wa tz.
 
Maranyingi serikali ambazo huondolewa madarakani huanza na mambo ya kishetani kama haya! Makosa ya kishetani kama haya yanaigharimu serikali ya CCM, makosa kama haya yanawafanya watanzania waungane kuwa kitu kimoja kuupinga ufedhuli na uharamia wa aina hii usiomithilika abadani! TUMUOMBEE KAMANDA Uli apone! Malafyale kyala akusaje!
 
Kama hali ni hii basi wananchi wote wake kwa waume kesho tuanze kukusanyika viwanja vya JANGWANI(TAHIR SQUARE) kuanzia saa 2 asubuhi ili kuilazimisha serikali iliyo madarakani kujiuzuru....Hii ni nchi yetu wote.
 
Wakati wananchi walikuwa wanasema CCM na serikali yake ni serial killer wananchi wengi hawakuamini,tuna madikteta wanaolinda utajiri wao na wana wao na wenzi wao kwa gharama ya damu za watu Mungu amewaaumbua Dr Ulimboka yuko hai na damu yake itakuwa tone la ukombozi ,Usalama wa Taifa waende wakatibu wananchi sasa
 
Huhitaji kuambiwa kuwa TUNAONGOZWA NA WAHUNI KWA HILI TUKIO (AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA). Time is very near to true democracy!!!
 
that insane who reporeted that the guy is not dead bahati nzuri mlimani tv walichukua picha wakati kamanda ulimboka anashushwa na wakati akipata kibano walimchukua na wameahidi kuwa watamwonesha mwanzo hadi mwisho.pia mkurugenzi wa mnh na mkuu wa emd prof mwafongo waligoma kutoa gari la wagonjwa la kwenda kumchukua uli.vile vile residents wa muhimbili wameitwa na uongozi wa chuo nadhani wanataka kuchimba biti warudi kazini
 
Kama hili ni lakweli na haya yakadhibitika kuwa ni ya kweli na hao waliofanya huu unyama walikuwa wametumwa na Serikali basi tumekwisha ya serikali yetu ni kweli alichokisema Mnyika.Katika njia ya majadiliano na suluhisho sijui hii ni Nguzo au ngazi ya ngapi?anayejua atujuze
 
Hayo yote myaonapo, changamkeni mkainue vichwa vyenu maana ukombozi wenu u karibu. Hii kauli aliitoa Bwana Yesu, bali leo naiandika ikimaanisha kuwa, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa watateswa na kuumizwa pamoja na damu zao kumwagwa, na waonapo hali hiyo ya kuonewa, ndio wajue kuwa ukombozi wao umewadia. Ni vivyo kwa kila mlalahoi wa Tanzania, damu zinazomwagwa leo hii zinaashiria kabisa kuwa ukombozi umekaribia. Hakuna ukombozi usio na tone la damu, kama ambavyo tone la damu haliwezi kumwagika pasi na ukombozi.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Back
Top Bottom