Pundit
JF-Expert Member
- Feb 4, 2007
- 3,733
- 123
Japokuwa kuzjiuzulu hakuji haraka na wala hatajiuzulu, yet ujumbe wa hii thread ni kuwa hajafikia malengo na matazamio ya wananchi. Kwa anayeweza kusoma katika mistari ya thread ilivyoanza, utajua tu kuwa watanzania wengi hawana tena matumaini na uongozi wa JK na kimsingi ni kuwa serikali iko likizo.
Mfumuko wa bei sasa unaumiza maisha ya watanzania ambao aliwaahidi maisha bora. kauli mbiu ya JK sasa haisemwi popote maana imepoteza maana. Kwa kura zetu, tusikubali tena kumweka madarakani JK hapo mwaka 2010.
Hata hivyo tufikirie namna ya kubadilisha mfumo mzima wa uongozi wa Tanzania ili tufikie malengo.
Mwanadiplomasia huyu anauma na kupuliza pande zote mbili.
Kwa hiyo MWK anatoa kauli za kisiasa za kuonyesha muelekeo? Nakubali kuna kauli za kisiasa za kuonyesha msimamo.Lakini hata serikali ya Tanzania ilipokuwa inalaani ubeberu wa siasa za kibaguzi za makaburu wa Afrika ya Kusini, serikali hii ilikuwa iko katika "Frontline States" na ilikuwa ina makambi ya wapiganaji wa ANC (Kongwa, Magadu, Dakawa etc) ambako condemnations hizi zilikuwa translated into action plans.
Sisi action plan yetu ya kumfanya JK ajiuzulu iko wapi? Au empty rhetoric?