A call for Kikwete to resign his presidency

A call for Kikwete to resign his presidency

Niliwahi kusema hapo awali kuwa hakuna jipya kwa Mh. zaidi ya kuendelea kutoa tabasamu lake. Wananchi hawahitaji tabasamu na ukenuaji meno wakati hawana uhakika wa kitoweo cha kesho. Mwananchi wa SUNUKA, KASULU, KIABAKARI, KITAGUTITI au na maeneo mengine utawaambia nini?? Watu walioko karibu na JK ndiyo wanazidi kujineemesha zaidi. SISIEMU yote haifai kabisa kutawala kwa sasa au baadaye. Watanzania wamechoka na wengine walishaanza kukata tamaa kabisa na maisha. Yeye jamaa haonyeshi kushtuka, DOWANS wanaendelea kulamba tu ile $ 152 kila siku. Mpaka sijui uchunguzi uishe au ripoti ipelekwe bungeni mjadili pamoja na UPUPU wenu wa kila siku pesa itakuwa ilishalambwa kwa sana. Na mnamjua huyo anayelamba, anaharakishiwa malipo yake kwa sababu yuko karibu na MUUNGWANA. JK mie nafikiri unatakiwa kurudi Chalinze ukaendelee na KILIMO cha MANANASI. Hiyo kazi naamini utakuwa makini kwa sababu utakuwa na uchungu na familia yako. Kwa sasa huna uchungu na WATANZANIA, kwani una tabu ya nini....... PENSHENI yako iko online once ukiachia ngazi.

Mkuu naona hii imefika wakati wake
 
He is a damn loser and if the constitution allows impeachment he should be impeached.The sooner the better.Our country is on the verge of being a failure state.

Amezidi porojo na safari.I think hiki kwake ni kipindi cha a tour of the world.
Damn you.
 
Baada ya kusoma alichoandika Mushi leo, imeonekana wazi kuwa mushi naye ataishia kama huyu hapa aliyeingia mtini baada ya kukosa washabiki kwenye huu utumbo alioweka hapa.
 
Kevo, kwenye nchi zenye katiba inayolinda maslahi ya nchi, huyu jamaa angeshapigiwa kura ya no confidence siku nyingi na saa hizi angekuwa ni history, lakini sisi tuna katiba inayolinda maslahi ya kundi la watu wachache ambao hata wakivurunda vipi wanaendelea kuwepo tu madarakani.

Mara nyingi Watanzania wametamka hadharani umuhimu wa kuwa na katiba mpya, lakini mafisadi hawataki kuruhusi hili maana wanajua ndiyo utakuwa mwisho wa ufisadi wao.
 
it is sad kujua kuwa Rais wetu wa sasa haondoki, hajiuzulu wala hana mpango huo, hizi ni kelele za mpangaji.
wala hana mpango wa kujitoa kwa wanamtandao.
Mtajiju!!
 
Baada ya kusoma alichoandika Mushi leo, imeonekana wazi kuwa mushi naye ataishia kama huyu hapa aliyeingia mtini baada ya kukosa washabiki kwenye huu utumbo alioweka hapa.

Mhhh, yaani wee MASAKA na MUSHI ... ehhhh watu weweee ahhh. Ngoja niwahi kamba BAFUNI ili NIJINYONGE maana nina wivu sana wa mapenzi yenu.
 
akiendelea kung'ang'ania historia itamhukumu tu...kwani hatuoni anacho fanya mpaka sasa.Hana hata barabara moja ya kujivunia aliyo maliza mpaka sasa....ameshindwa kazi apumnzike tu awapishe wenye uwezo aliowabania.
 
Wana JF
Kwa taarifa ni kwamba wachina walitabiri kuwa JK atakuwa rais pekee wa TZ ambaye ataserve kipindi kimoja tu.
Hao ni wachina.

Kuna mchakato umeanza wa kumuondoa JK mara baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza na ndio maana hata kwenye kikao cha juzi cha NEC ameshindwa kuvumilia na kusema watu bado wanautaka urais.
UKIONA MTU MZIMA ANALIA UJUE KUNA JAMBO.
 
Kikwete ameshindwa kufanya kazi yake kama raisi wa jamhuri ya Tanzania na amirijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Tanzania. Katika hili, nini tena kinaweza kusemwa juu yake?
 
MWKK umeamka? karibu ukumbuni. na tunatarajia yaliyokuficha kwa kipindi hichi yamepita salama
 
maboksi hayeshi.......tumefurahi kuweza kujumuika hapa kutupa mchango wako
 
Jk historia ya tanzania itamuhukumu kuwa aliwahi kuwa kiongozi wa Tanzania ambaye hakuwa na msimamo dhabiti kama RAIS. hakuweza kutumia sheria tulizonazo katika kuwakomboa watanzania.

wale waandishi wa vitabu nafikiri kuna hoja za kutosha kuweza kuandika kitabu cha Historia ya marais wetu, Mkapa tayari tuna kila issue yake, Ila sasa JK anaelekea kuwa kiongozi wa ajabu sana baada ya kushindwa hata kulinda masirahi ya watanzania na kuacha wezi kuendelea kutembea kwa kujidai.

Mwalimu amekuwa mwandishi mzuri sana wa vitabu, watanzania tumuenzi kwa kuandika vitabu kwa ajiri ya vizazi vijavyo. Hapa JF tuna information za kutosha kuchapisha vitabu mbali mbali vya historia za nchi yetu. Wale Mangungo lazima wakae kwenye vitabu vikubwa na viuzwe kimataifa.

Kwa sababu ya watu wanaotumia hila tunaweza tusipate uhuru hivi karibuni lakini lazima tuwe na historia za harakati katika kuelekea uhuru kamili, tusisahau wale waliopotea katika kupigania uhuru huu.
 
Kikwete ameshindwa kufanya kazi yake kama raisi wa jamhuri ya Tanzania na amirijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Tanzania. Katika hili, nini tena kinaweza kusemwa juu yake?

Mkuu,

Hivi majuzi, heroin wako, Anne Malecela, amemu endorse Rais Kikwete.

Je alichemsha?

Context ya alichosema: Alikwenda kwenye radio ya Mwanakijiji kusema kwamba Kikwete ni kiongozi mzuri dhidi ya ufisadi kwa sababu alitoa spichi miaka miwili iliyopita akisema hana ubia na mtu, na kwamba mikataba ya madini ipitiwe.

Nakuomba kwa taadhima zote, Mwafrika wa Kike, unipe jibu kutoka moyoni mwako, kwa mapenzi yako ya kweli kwa Tanzania. Ndugu yangu unajua ninavyoheshimu ushupavu na ukakamavu na umahiri wa kichwa chako. Nakuomba ukusanye nguvu kunijibu hilo swali kwa kiapo juu ya nchi yako na bibi yako -(kama Wamarekani wanavyo apia!)
 
Mkuu Kuhani

Mimi nitakujibu hata kwa hili maana kama mwanasiasa wewe ulitegemea asemeje? na baada ya kusema unavyofikiria ulitegemea nini? Nitashangaa kama ulitegemea jibu tofauti kama alivyosema.

Mkuu inawezekana hujui siasa za nchi zinazoendelea. tanzania siyo UK au marekani
 
Mkuu,

Hivi majuzi, heroin wako, Anne Malecela, amemu endorse Rais Kikwete.

Je alichemsha?

Kwanza kabisa sijui una maana gani unapomwita mama Malecela - heroin.

Kuhusu kuchemsha kwa Mama Malecela kumu-endorse Kikwete itategemea na mtizamo wako.

Kuna watu hapa US wanaamini kuwa Kerry, Edwards na Ms Clinton walikosea kupiga ile kura ya kumpa Bushi authority ya kuivamia Irani. Kuna wengine bado wanasema kuwa kulikuwa hakuna makosa yoyote kwa kupiga kura ya ndiyo.

Chris Mathew wa NBC anaamini kuwa ile kura ndiyo ilimfanya Clinton akose nomination iliyoisha ya Democrats ingawa wengine wanaona vinginevyo - hii yote ni mitizamo.

Mama Malecela yeye kwa mtizamo wake anaona Kikwete amefanya mengi kwenye kupigana na ufisadi - kuwatosa Lowasa na Mramba. Mimi naona kuwa kikwete ameshindwa kufanya kazi kwa hiyo aresign. - Hii pia ni mitizamo.

Siwezi kuhukumu mtizamo wa Mama Malecela, kwa sasa ninahukumu vitendo vyake ambavyo so far niko very impressed.

Context ya alichosema: Alikwenda kwenye radio ya Mwanakijiji kusema kwamba Kikwete ni kiongozi mzuri dhidi ya ufisadi kwa sababu alitoa spichi miaka miwili iliyopita akisema hana ubia na mtu, na kwamba mikataba ya madini ipitiwe.

Ukiangalia alichosema Mama hapa ni kweli - Kikwete alisema kuwa hana ubia kwenye serikali na pia alisema kuwa mikataba ya madini itapitiwa. Yote haya yalitokea. Sasa kama yamefanyika kinafiki (mtizamo wangu) au la, hilo ni swali kubwa sana.

Nakuomba kwa taadhima zote, Mwafrika wa Kike, unipe jibu kutoka moyoni mwako, kwa mapenzi yako ya kweli kwa Tanzania. Ndugu yangu unajua ninavyoheshimu ushupavu na ukakamavu na umahiri wa kichwa chako. Nakuomba ukusanye nguvu kunijibu hilo swali kwa kiapo juu ya nchi yako na bibi yako -(kama Wamarekani wanavyo apia!)

Mkulu wangu hakimu, mimi nilikuwa Tanzania karibuni. Watanzania wengi sana wanasikiliza bunge. Huko vijijini watu wengi wanafurahia sana wakiona wabunge wakiihoji serikali kwa ukali (kitu ambacho kilikuwa kimeanza kupotea) na wengi wanapata habari nyingi kwa kusikiliza maneno ya kina Mama Malecela.

Mimi ni ombi langu kama wakipatikana wabunge wengi ndani ya ccm kama Mama Malecela. Nitaunga mkono mapambano yake badala ya kumdemonize hapa jamvini na kwingine kokote.

Asante
 
Back
Top Bottom