Kwa kweli hata mimi inanishangaza kuona watu wazima ambao nina imani wana upeo mkubwa wa kuchanganua mambo,ghafla wanakurupa kama walevi wa pombe za kienyeji kuleta hoja isiyojadillika humu.Ninafahamu suala la uhuru wa kuongea,lakini basi ebu tuwe tunajaribu kutoa hoja ambazo angalau tudhani zinaweza kuleta changamoto za maana.Ndio,najua mtoa hoja lazima awe ni mpinzani,sawa, naliheshimu hilo.Lakini hata kwa wapinzani makini sio rahisi ukisikia wakitoa mapendezo mfu kama ya huyu mama.Sasa,nakuhakikishia wewe na wale wote wanauunga mkono kwamba mpende msipende JK ni Rais mpaka 2015.Kama humtaki,basi hilo ni tatizo lenu binafsi.
Na lazima tuelewe kwamba JK amesimamishwa na CCM ili kusimamia ukelezaji wa Ilani ya CCM.Na hilo ndio analolifanya.Sasa kuanza kumlaumu kwamba eti hana mikakati ni upofu wa kujua masuala ya utawala wa nchi.Sasa,kama mtu ana hoja ailekeze kwa CCM yenye ilani(ambayo ndio mikakati yenyewe).Tusitake kumuonea mtu hapa.CCM ndiyo inayotawala na wala sio JK.Sasa kama mna ubavu, basi,iambieni CCM kuwa iachie hatamu ya uongozi.Sio haki kumlenga mtu wakati hatamu ni ya chama.Msipende kuropoka tu ila mradi mna uhuru wa kufanya hivyo.Muwe mnapima mambo na kuyatafakari kwa kina.