Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Lol!!! Watu wengine wanachekesha kweli. Sasa wewe hoja yako iko wapi? Au kuandika kwa mihasira ndiyo hoja yenyewe!!!
Unapenda kukurupuka sana wewe.
Hoja ni kwamba rais hana uwezo wa kuliongoza taifa hili au ameshindwa kutimiza yale aliyotuahidi.
1.Kupambana na Rushwa
Kashindwa kushughulikia wezi wa EPA.
Kashindwa kuzuia upotevu wa fedha nyingi uliowahusisha marafiki zake kupitia Kampuni yua Richmondi
Kapiga hatua za mbali zaidi kumtetea mtangulizi wake anayekabiliwa na tuhuma za rushwa yaani Benjamini Mkapa.Hii moja kwa moja inapingana na dhamira yake ya kweli ya kuupinga ufisadi
No. 2. Kashindwa kutumia muda wake vizuri ofisini na kuacha kuzurura huku na huko,ili aweke mikakati mizuri ya kupunguza gharama za safari zake kila kukicha na badala yake awatumie mabalozi wetu nchi za nje kutekeleza majukumu yasimlazimu rais kufuatilia huko.Huu ni ubadhiri ambo moja kwa moja unapingana na dhamira yake ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania
No.3. Kashindwa kuilinda katiba ya Tanzania inayokataza watu kupewa nyadhifa kiubaguzi.Kuwateua marafiki zake kwenye taasisi za umma example,Rweza Mukandala wa UDSM ili kutekeleza matakwa yake binafsi ni matusi makubwa kwa katiba yetu.He must GO!
No.4. Kushindwa kwawajibisha watumishi wa serikali ambao ni wzembe kazini na kufikia hatua ya kuwatetea ni kaosa kubwa
hizo ni chache,wazalendo wengine watakupa hoja nyingine zaidi.Na wewe mkuu na wenzako toa hoja zenu ni kwanini huyu Rais aliyeshinwa asijiuzulu?