Nini faida na hasara ya Tume ya Uchaguzi?

Ossaessa

Member
Feb 22, 2020
17
9
Salam wana JF

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wananchi, wanasiasa, viongozi wa dini, taasisi mbalimbali pamoja na baadhi ya Viongozi wastaafu kutaka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, 2020. Upande wa pili kumeibuka kundi linalopinga uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Oktoba mwaka 2020. Kundi hili limejaa wanasiasa watupu hususan wa Mrengo fulani.

Hoja ya kundi la kwanza imejikita kwenye haki, wanasema Tume Huru ya Uchaguzi itasimamia uchaguzi ulio huru na haki na kuondoa kasoro kama zilizojitokeza kwenye chaguzi ndogo za marudio na ule wa Serikali za Mitaa. Wanakazia hoja yao kwa wakurugenzi ambao ni wanachama wa chama fulani kinachoshiriki Uchaguzi na ni wateule wa mmoja ya wagombea kusimamia uchaguzi hauwezi kuwa huru na wa haki. Upande wa pili unaopinga tume huru hoja yao wanasema huu sio wakati wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi.

Wanaenda mbali kwa kusema kama tume sio huru mbona wapinzani wanashinda?

Nihitimishe kwa kuuliza nini maoni yako juu ya Tume Huru ya Uchaguzi in faida gani au hasara gani kwa taifa letu?
 
Kabla ya kujua faida na hasara, ningependa kujua Muundo wa ''tume huru''!

Naomba kuelimishwa kwa sababu kuna wengine tunaimba ''tume huru'' lakini hatujui hata muundo wake!
 
Faida ya tume huru ni kwamba;

1. Itaendesha mchakato wake bila kuingiliwa na dola

2. Itakuwa neutral na fair zaidi katika utendaji wake

3. Matokeo na mchakato mzima wa uchaguzi utakuwa wa kuaminika zaidi kwa kuwa utakua wazi.

4. Itaondoa manung'uniko ya waathirika wa mfumo uliopo ambao kiasi kikubwa unaathiriwa na maagizo pamoja na ushawishi wa fedha.

5. Itaimarisha utulivu nchini, kwa kuondosha tatizo la imani hafifu juu ya utendaji wa tume iliyopo

6. Rushwa katika uchaguzi itapunguzwa zaidi hasa kwenye mchakato wa upembuzi wa majina na upitishwaji.

7. Etc....... (angalia kipengere cha etc)


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Agizo, nimekuteua mimi, mshahara ninakulipa mimi, nyumba nimekupa mimi na gari nimekupa mimi, tume lazima itekeleze agizo hili hivyo haina sifa ya kusimamia uchaguzi.
 
Back
Top Bottom