Kwanza naomba Mods, uzi huu usiunganishwe na nyengine.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kauli mbali mbali kuhusu Madai ya tume huru ya uchaguzi Tanzania.
Si vyama vya upinzani tu lakini hata wadau wa maendeleo na demokrasia wamesikika wakihimiza kwa serikali kuleta tume huru ya uchaguzi KABLA YA KUFANYIKA UCHAGUZI
Aidha serikali imeahidi kufanya uchaguzi wa uwazi, huru na haki kupitia kauli za Mh Rais alipozungumza na Mabalozi wakati wa chakula cha pamoja kuukaribisha mwaka mpya, Waziri Mkuu Bungeni, waziri wa mambo ya nje kule UN na waziri wa mambo ya Ndani alipozungumza na Kaimu Balozi wa Marekani hivi karibuni.
Katikati ya maelezo hayo kutoka kwa wakubwa hao, pia alisikika Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru akieleza maelezo ambayo yana ukakasi mkubwa . Hata waziri mkuu naye ufafanuzi wake una ukakasi. Kusema tume iliyopo ni huru huko ni kujitia pamba za sikio.
Suali linakuja hii ahadi ya Serikali kufanya uchaguzi huru na haki ni kwa tume iliyopo au kuna nini?
Kwa mtazamo wangu ikiwa hakukufanywa marekebisho yoyote katika muundo wa Tume na mfumo wake wa ufanyaji kazi basi hakuna Tume huru na katu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
CCM na Sereikali yake waTAMBUWE KWAMBA WADAU WANADAI TUME HURU KWA SABABU HII ILIYOPO HAIKO HURU.
Kushupalia vifungu vya sheria na kunukuu kwa ustadi kuhusu uhuru wa tume iliyopo hakusaidii kitu ikiwa mfumo wa uteuzi na uwajibikaji uko kwa mtu hilo ni tatizo
Kukosekana kwa Tume kuhojiwa na kuwajibishwa mahakamani hilo nalo ni tatizo.
MWISHO
Serikali kushindwa kutoa ufafanuzi wa Uchaguzi huru na haki NA HATUA ZIPI ITACHUKUWA ILI WADAU WAWEZE KUPIMA KAMA KWELI KUNA NIA HIYO ni kama inavizia na kuweka hadaa kwa wadaU HAO. hAPA KUNA KILA ISHARA YA ULAGHAI.
Uchahguzi huru na haki ni Process, huwezi kusubiri hatua ya mwisho ndio usaeme uchaguzi ulikuwa huru wakati hatua muhimu zote hazina uwazi na ushirikishwaji.
Serikali itoe ufafanuzi wa wazi inakusdudia kufanya nini. Huu ni mwezi wa Pili mwishoni kuelekea wa tatu, itakuwa imebaki miezi saba tu na hatua nyengine muhimu za uchaguzi zinaendelea.
Kwa ufupi kuna ahadi ya Uchaguzi huru na haki kwenye mazingira yasiyoruhusu.
Serikali itoe ratiba ya hatua za kufanya uchaguzi huru na haki na ufafanuzi unaojitosheleza.
Bila kufanywa marekebisho ya muundo na mfumo huko ni kulaghai watu.
Kinachotakiwa ni Tume Huru ya Uchaguzi ili kupata uchaguzi huru na haki na wala sio ahadi ya uchaguzi huru na haki katika mfumo usioruhusu haki kupatikana.
Ni hayo tu
Kishada.