Tume ya Uchaguzi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
FB_IMG_1582626481002.jpg


Huyu mtu mmoja kwanini ana vitambulisho viwili ?
 
hili lilinitokea mwaka 2015.. kwenye daftari nikakuta kuna majina yangu mawili.. nikuzuiliwa kupiga kura na kadi ikachukuliwa.. mwaka huu nimewafata nikafuta jina moja na jingine ndo nikapewa kitambulisho. so usiwe na mawazo..
ngoja tusikie kutoka NEC
 
Hapo mwenye kosa ni huyo kijana

Inawezekana alienda kujiandikisha mara ya pili kwa kuripoti amepoteza kitambulisho
Wacha kusema uongo hizo ishu za kujiandikisha vituo viwili tofauti hufanywa na ccm tangu miaka ya 1995 zoezi hilo mulilianzisha Zanzibar mpaka sasa munalitumia hutumia vikosi vyenu vya mazombi na majanjawiri mwaka 2015 walitoka vijana unguja wakaja kupiga kura Pemba watu wakawashtukizia wakawapiga wakawa hali mbaya usiku balozi seif Ali idi alikuja kuwachukua kwa ndege na kurejeshwa unguja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1368813

Huyu mtu mmoja kwanini ana vitambulisho viwili ?

Hili nalo linahitaji tume ya uchaguzi kusema kweli wewe soma vizuri hapo chini utagundua hapo kuna cha zamani na cha sasa! Hapo ni wazi hapo kimoja kimebadilishwa kinarudishwa na amepewa kipya ambacho amehamia kituo kipya cha kupigia kura!

Mwanzo alikuwa kituo kingine na sasa amebadilisha makazi hivyo amejiandikishia kwenye kituo kipya na automatically kituo cha mwanzo jina lake halitokuwepo bali litatokea kituo cha sasa alicho jiandikisha upya!

Hapo mbona hakuna kipya?
 
kama elienda kujiandikisha mara mbili.. kosa hapa ni la wao waandikishaji.. system ilitakiwa iseme mbona upo kwenye system.. angepewa tu kadi kwa namba ileile ya iliyopotea.. na si kumpa kadi mpya yenye namba tofauti
... umemaliza Mkuu. Kawe Alumni, soma hiyo.
 
Kweli hapa tunahitaji ufafanuzi wa kina..vinginevyo hili daftari halina maana - tutaliamini vipi?
 
Hapo mwenye kosa ni huyo kijana

Inawezekana alienda kujiandikisha mara ya pili kwa kuripoti amepoteza kitambulisho
Huwezi kujiandikisha mara mbili. Ukitaja tu jina inaonekana kama ulishajiandikisha au la. Mimi changu kilipotea walipokuja nikataja jina chap kikajitokeza kikachapwa sababu sikuwa na mabadiliko niliyofanya. Sasa itakwaje majina mwaka kila kitu kiko sawa isipokuwa makazi tu ndio tofauti kitoke mara mbili? Vitambulisho vyote viko kwenye database hiyo hautegemewi kuwa na makosa kirahisi hivyo. Nenda kokote nchi hii database ikifunguliwa unaonekana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom