Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaongeza siku za kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Besta Mlagila

Senior Member
May 29, 2018
101
191
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza siku tatu za zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Zoezi hilo lililokuwa lifikie tamati leo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani sasa litafikia tamati Jumapili February 23 Mwaka huu.

=====
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (Nec) imeongeza muda wa siku tatu katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dar es Salaam uliotarajiwa kufikia ukomo wake leo Alhamisi Februari 20, 2020.

Uboreshaji huo ulianza Februari 14 na leo ndio ilikuwa siku ya mwisho lakini tume hiyo imeongeza siku nyingine tatu mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 15(1) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura namba 343 pamoja na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura namba 292.

"Kwa hiyo Ikifika tarehe 23, 2020 siku ya Jumapili hatutaongeza muda tena," amesema Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo, Dk Wilson Charles.

Katika ufafanuzi wake, Dk Charles amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia vyema muda huo.

Kwa mujibu wa tume hiyo, vituo 37,814 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo kwa Tanzania bara na visiwani.

Chanzo: Mwananchi
 
Tayari nimekamilisha zoezi, nimepata kitambulisho changu kipya.

Serikali makiini kabisa hii.

Na utaratibu ni mzuri kabisa pongezi kwa NEC.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imeongeza siku tatu za zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa za wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Zoezi hilo lililokuwa lifikie tamati leo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani sasa litafikia tamati jumapili February 23 Mwaka huu.
Baada ya Chadema kuomba wanataka wawaoneshe kuwa Tume iko huru na sikivu.
 
1-640x400.jpg


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeongeza muda wa siku tatu katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura katika Mkoa ya Dar es Salaam uliotarajiwa kufikia ukomo wake leo Februari 20, 2020.
 
Tume Huru ikipatikana na katiba mpya inayoruhusu kupinga matokeo ya Rais Mahakamani...nikumbusheni mwaka huo nitajiandikisha....
 
Back
Top Bottom