Tume Huru ya Uchaguzi itaundwa pale tu CHADEMA na wapinzani kwa ujumla watakaposusia Uchaguzi Mkuu 2020

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kabla ya uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, nilipost uzi unaosema kuwa CCM wameweka mapandikizi yao yagombee lakini niliishia kupigwa BAN ya miezi mitatu na hawa moderator mpaka uchaguzi ukaisha bila bila.

Sasa leo nawaambia hivi, CHADEMA na upinzani kwa ujumla mnatakiwa kutoa tamko la kususia uchaguzi mkuu 2020 endapo tume huru haitaundwa.

Nawahakikishia kuwa WAKATI NI SASA, mtakuja kujuta huko mbeleni pale mtakaposema BORA TUNGEJUA.

Ni vema uchaguzi ukafanyika hata mwakani 2021 kukiwa na tume huru yenye maridhiano kuliko kufanyika mwaka huu kwa kutegemea FAIR PLAY ya tume iliyopo.

Msipogomea uchaguzi mkuu, HAMTOBOI.
 
Wakipatikana hata Wabunge kumi (10) wa upinzani Bunge bado watapewa nafasi ya kuikosea serikali na kuleta matokeo chanja kuliko wabunge wote kuwa upande wa kusifia tu.
 
Wakipatikana hata Wabunge kumi (10) wa upinzani Bunge bado watapewa nafasi ya kuikosea serikali na kuleta matokeo chanja kuliko wabunge wote kuwa upande wa kusifia tuu.
Hali ilipofika sasa hivi si ya KUBETI matokeo.

Ni ama upinzani uchukue nchi au wawaachie CCM watawale peke yao. Sasa hapo ndo utaelewa impact yake
 
Ni kweli mfumo wa uteuzi na uundaji wa tume yetu ya uchaguzi ya sasa hauendani na mazingira halisi ya matakwa ya mfumo wa vyama vingi! Haiwezekani Kiongozi mkuu wa chama cha siasa kinachoshindana na vyama vingine tena kwa kumsimamisha yeye mwenyewe kushindana na wagombea wa vyama vingine alafu yeye huyohuyo akawa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Tume ya uchaguzi na kuwalipa mshahara watendaji wake alafu hapohapo tukategemea uchaguzi uwe huru na wa haki kwa vyama vyote!

Suala hili lazima lifanyiwe marekebisho sambamba na kuweka kipengere cha kupinga matokeo ya rais mahakamani! Sote tukilijadili jambo hili kwa mtazamo chany,a hasa wa kupenda haki na kulinda amani yetu, tutakuwa tumeisaidia sana hata CCM ambayo kwasasa hawapendi habari hizi kwa kujidanganya kuwa kamwe hawatakujakuwa chama cha upinzani, lakini upepo wa siasa huwa unabadilika, na huko tuendako lazima kuna chama cha upinzani kitakujashika dola!

Tukubali tusikubali tunahitaji mabadiliko ya tume ya uchaguzi kama kweli tuna nia njema ya kuilinda amani ya nchi yetu kwa maendeleo ya taifa letu! Hivyo ni bora tukaachana na kila kitu kwanza tuliweka jambo hili katika mstari unaotakiwa!
 
Trust None, Hata mimi sioni logic ya kugomea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana halafu unakubali kuendelea na uchaguzi mkuu. Unless wamepanga kususia last minute. It's between a rock and a hard place!

Wakisusia dakika za mwisho CCM watafanya kama mwaka jana, watajipitisha "bila kupingwa". Wakijitoa sasa, CCM kupitia Msajili, itavifuta vyama vyao ili vikose ruzuku ya kujiendesha.

Hii sio 'goli la mkono' bali ni 'ushindi wa mezani'. Yaani mpira uchezwe au usichezwe mshindi kesha julikana!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trust None,
Hapa ndipo watanzania tunapokwama kila jambo kuwaachia Chadema! Uchaguzi si wa vyama ni wa wananchi wote waliondani ya vyama na wasio na vyama kila mmoja wanataka kura yake iwe haki yake iheshimiwe na si vinginevyo.

Madai ya tume huru yanatokana na raia ambao si wazalendo na hawatii sheria kwa vitendo vyao vya kutoheshimu sheria ya kura yako ni haki yako iheshimiwe, wangetii kusingekuwa na sababu ya kuwa na tume huru.

Watanzania wote tunataka kura tunazopiga ndizo zihesabiwe kama zilivyo na zitupe viongozi kulingana na tulivyopiga na si vinginevyo kwa mtindo wa goli la mkono.

Ndugu yangu badilika uone kura yako ni haki yako iheshimiwe na waliopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi, uchoyo na urafi ni dhambi.
 
Hii tume ya sasa ni 100% pro-ccm na hilo ni punguani tu ndiye anayeweza kubisha. Hii tume ni ya watu tu wanaopewa amri na rais na kufuata mara moja bila kuhoji.

Magufuli hana record ya kuheshimu demokrasia na hilo liko wazi ukifuatilia zama zake za ubunge, wa kule Chato wanalielewa hili, anapogombea kitu waga hataki agombee na mtu.

Ktk nchi hii CCM haijui inakubalika kwa kiasi gani na hili linasababishwa na kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi kwani matokeo ambayo yamekuwa yakitolewa na hiyo tume yamekuwa ya kubumba mno kwa muda mrefu sasa.

Kwa hii tume ikiwa ulingoni ukiongeza na Magufuli mwenyewe pembeni sambamba na maaskari wake, naona kama kiama ya upinzani inakuwa imewadia.

Upinzani wa vyama unatoweka na upinzani unaenda "Underground" ambayo ni hatari sio tu kwa mtawala mwenyewe lkn hata kwa ustawi na mshikamano wa taifa.
 
Trust None,
CCM wanajua fika kwamba ukishagusa Katiba ama ukafumua Tume ya Uchaguzi basi watakuwa wanaelekeza kichwa chao kibra...

Kwa wapinzani wote wahakikishe wanadai tume hii kwa njia zote bila kivunja sheria za nchi..

Suala la kususia uchaguzi lina ukakasi; yaani shamba unataka kumsusia ngedere...mwisho wa siku mabua ni halali yako.
 
Je chadema ikisusia vyama vingine vikashiriki si itakuwa kama ule wa serikali za mitaa?

CHADEMA wasiposhiriki hata hivyo vyama vingine vitajitoa 1. Ni kutokana na kukwepa aibu ya watu wachache watakaojitokeza kupiga kura. 2. Iwapo CHADEMA watatangaza kutokushiriki CCM ni rahisi kuhonga hivyo vyama vingine visishiriki ili ipite bila kupingwa kwani serikali haina pesa, hivyo wakiweza kusave pesa za uchaguzi kwao itakuwa ni baraka.
 
Kilio, kilio, ni kilio cha kudai Tume Huru ya Uchaguzi Mkuu, kutoka kwa karibu viongozi wote wa vyama vya upinzani. Maswali kadhaa yanajitokeza:

1) Je, kuna haja ya kuwepo kwa hiyo tume?
2) Je, Tume ya Uchaguzi iliyopo ina mapungufu gani?
3) Hiyo Tume Huru inapaswa kuwa na vigezo gani?

Pamoja na kupata tafsiri sahihi ya Tume Huru ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na vigezo vyake, Serikali itumie busara kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi. Kutekeleza hilo kutaziba mianya ya wanasiasa kuweka kwapani mpira wa uchaguzi, siku ya siku.
 
Tume ni Huru. Nyingine ya nini? Ushauri wangu kwenu, jiandaeni kwa uchaguzi. Mkibaki Tume Huru, Tume Huru, mtashtukia uchaguzi huo na hamjajiandaa. Shauri yenu!!!!
 
Back
Top Bottom