uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. JamiiForums Tanzania CHADEMA mpaka sasa sielewi mipango yao uchaguzi mkuu ujao

    Mpaka sasa hakuna tamko rasmi la mwenyekiti Mbowe kuhusu uchaguzi mkuu unaokuja ni vyema viongozi wakatoa tamko kama watagomea kushiriki uchaguzi mkuu au wapo tayari kuingia kwenye uchaguzi hivyo hivyo bila katiba mpya ama tume huru ya uchaguzi.
  2. JamiiForums Tanzania Kwanini Watumishi wa Umma wanaendelea kutumika kwenye Uchaguzi licha ya Mahakama ya Afrika kuitaka Tanzania kubadili kifungu hicho?

    Moja ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa demokrasia nchinina kitendo cha Tume kutumia watumishi wa umma katika michakato ya kiuchaguzi. Kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Mswada, Tume itaendelea kutumia aukuazima watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi, kwa lugha nyingine...
  3. JamiiForums Tanzania Kupitia ilani ya uchaguzi ya 2020-2025, CCM iliahidi, inathubutu kutekeleza na inasonga mbele

    Ukiangalia na kufuatila kwa makini. Kwa kiasi kikubwa sana, mpaka sasa, Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 imetekelezwa kikamilifu kwa weledi na umahiri mkubwa sana. Hili liko wazi na halina ubishi. Kwa muda mfupi uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu2025, CCM inatarajia kuvuka lengo na kuvunja...
  4. JamiiForums Tanzania Kampeni za Uchaguzi zimeanza DRC, Fomu ya Urais Tsh. Milioni 150

    Wakati wagombea urais wa Tanzania wakitoa Sh5 milioni kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano, kwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wagombea urais wanatakiwa kuonyesha risiti ya malipo ya faranga za Congo milioni 160, sawa na zaidi ya Sh150.3 milioni kama ada zisizorejeshwa kwa Tume Huru ya...
  5. JamiiForums Tanzania Makonda ana hulka zile zile za Magufuli. Uchaguzi ujao tegemeeni yale yale ya 2020

    Tegemeeni yale yale, msikenue meno mkasema kutakuwa na unafuu uchaguzi ujao! Msijidanganye kwamba kuna jimbo mtapata, Msidhani Makonda kateuliwa kihasara hasara, hawa wameangalia mtu mwenye roho ngumu, na asieogopa chochote. Huyu amewekwa hapo kuwashughulikia kisayansi, huyu ni Magufulism...
  6. R

    JamiiForums Tanzania Taja jimbo unaloona linakwenda upinzani 2025 endapo Tume ya Uchaguzi itakuwa ya haki

    Natafakari upya kuhusu wabunge mzigo kwa jamii. Safari hii najiuliza majimbo gani yatakwenda upinzani? Wanasiasa wapya watakuwa akina nani?
  7. JamiiForums Tanzania Watanzania tunasubiri kuibiwa kuelekea uchaguzi mkuu 2025

    Uchaguzi ni gharama kubwa sana kwa wagombea, vyama vya siasa na taifa kwa ujumla wake. Kupata pesa za kugharamia kupita kwenye kura za maoni, kupiga kampeni, kuchaguliwa, kulinda kura na kutangazwa kuwa mshindi ni bei kubwa sana. Watanzania tunatarajia kusikia wizi au uhalalishaji wizi mkubwa...
  8. JamiiForums Tanzania Je, wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni batili? Ni mvinyo wa zamani, kwenye chupa mpya? Why ubatili huu?

    Wanabodi, Kama kawa, leo nimepata fursa kuwaletea makala elimishi ya uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa swali Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili? Je, muswada huu ni mvinyo ule ule wa...
  9. JamiiForums Tanzania Tujadili kifungu 47(3) cha Muswada wa sheria ya Tume ya Uchaguzi

    Nimeona hiko kifungu cha 47(3) kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kufanya maamuzi ya nani apige wapi kura siku ya uchaguzi wa Rais.... Watanzania mnakionaje hiki kifungu? Kinasherehesha haki au ndiyo tunaingizwa mkenge kama wa DP World?
  10. JamiiForums Tanzania Vyama Vya Siasa Vyasema Kusoma kwa Muswada wa Sheria ya Uchaguzi ni Ishara Nzuri

    Siku moja baada ya kusomwa kwa muswada unaokwenda kutunga sheria mpya itakayoanzisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakayojitegemea, Vyama vya siasa vimesema ni ishara nzuri ya kuelekea kuwa na uchaguzi huru na haki. Wakati hilo likifanyika pia vyama vimesema umefika wakati sasa wa kuhakikisha...
  11. JamiiForums Tanzania Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

    Wanabodi, Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Makala ya leo ni kuhusu fursa ya kuufanya uchaguzi Mkuu ujao wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Kwanza tukubaliane katika uendeshaji wa nchi...
  12. R

    JamiiForums Tanzania Nimesema tujiandae kisaikolojia kuhusu miswada ya leo bungeni, Kila kitu anachagua Rais tume ya uchaguzi directly or indirectly

    Tume huru ya uchaguzi iko wapi ikiwa kila kitu anachagua rais? directly or indirectly At least nilitegemea kitu kama hiki..... to say the least Pascal Mayalla Erythrocyte johnthebaptist 20. The Swedish Election Authority is organised as follows: 21. The Election Authority is governed by a...
  13. JamiiForums Tanzania Miswada miwili ya sheria za uchaguzi yatua bungeni

    Leo tarehe 10 novemba 2023, Bunge limesoma miswada miwili ya sheria za uchaguzi kati ya miswada mitano iliyosomwa kwa mara ya kwanza. Miswada hiyo kuhusu sheria ya uchaguzi kwa mujibu wa bunge ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; na Muswada wa Sheria ya...
  14. M

    JamiiForums Tanzania Zitto Kabwe: ACT Wazalendo imehujumiwa wazi uchaguzi wa Mtambwe

    Hii ni kali. 👇 "Tumeshuhudia hujuma za wazi Uchaguzi wa Mtambwe; tena katika wakati ambao nchi ipo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK), wananchi wametulia na ipo Kamati ya Maridhiano ya Vyama vinavyounda SUK. Haikutarajiwa uhuni huu katika zama hizi."
  15. JamiiForums Tanzania Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?

    Wanabodi, Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kwa Maslahi ya Taifa, ambazo ni kuhusu jambo lolote la Kisiasa, Kiuchumi au Kijamii . Bandiko la leo ni bandiko muendelezo Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na...
  16. JamiiForums Tanzania Tukiwa tunaelekea Uchaguzi mkuu, sasa hivi kila Mbunge anajifanya kuiponda Serikali

    Siku ya jana na Leo Bunge limekuwa la moto kweli, kila mbunge akiishambulia serikali na mawaziri wake. Kwa sisi wenye uelewa tunajua hizi ni mbio za sakafuni tu. Sasa hivi wabunge wanajua Muda wa kukaa bungeni umeisha, kila mbunge anajinadi sasa na kuishtumu serikali juu ya ubadhirifu wa fedha...
  17. K

    JamiiForums Tanzania Jibu kwa Tundu Lissu: Njia nzuri ya kuzuia uchaguzi ni kuruhusu uchaguzi ufanyike

    Kuna mada iliyowasilishwa humu JF ikidai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kaeleza kwamba endapo Katiba Mpya haitapatikana kabla ya chaguzi zinazofuata 2024/2025, juhudi za kuzuia uchaguzi huo usiwepo zitatumika kuuzuia. Kauli hii imesikika kwa muda kitambo sasa, tokea ndani ya chama hicho...
  18. JamiiForums Tanzania Tetesi: Uchaguzi TCCIA Wa 07.11.2023 wadaiwa kuingia dosari za kujazia fomu kutokea ndani ya kamati ya uchaguzi na menejimenti

    Mimi Tai katika kupaa kwangu nimekutana na penyenye kuwa Uchaguzi wa TCCIA unaofanyika tarehe 07.11.2023 umeanza kupata dosari. Viongozi wa Makao Makuu wameanza kupanga safu, ikiwa ni pamoja na kujazia fomu wagombea ambao hawakuomba nafasi hizo hadi zoezi linafungwa. Penyenye hii inasema...
  19. R

    JamiiForums Tanzania Maoni: Ifanyike tathmini ya Uchaguzi wa 2019/2020 kabla ya kufanyika uchaguzi 2024/2025

    Salaam, shalom. Baada ya kumsikiliza Kwa makini Mzee WARIOBA akihojiwa katika kipindi Cha Dakika 45 kituo Cha ITV, Kuna mambo nimeyatambua Mzee anajaribu Kutoa angalizo na umuhimu wa Serikali kutathmini kilichojiri 2020 Ili kuepuka KURUDIA changamoto zile zile. Mzee Warioba amejaribu kuongea...
  20. B

    JamiiForums Tanzania Lissu: Hakuna Katiba Mpya, hakuna uchaguzi

    HIzi ndiyo zile kauli tunazozitaka kuzisikia toka kwa viongozi wetu katika mapambano: HIzi ndizo zile kauli wanazozielewa vyema CCM na vibaraka zao. HIzi ndiyo zile kauli za watu, yaani kauli za wananchi. Kauli ya wengi ni kauli Mungu. Aluta continua!
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…