Jibu kwa Tundu Lissu: Njia nzuri ya kuzuia uchaguzi ni kuruhusu uchaguzi ufanyike

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,663
8,809
Kuna mada iliyowasilishwa humu JF ikidai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kaeleza kwamba endapo Katiba Mpya haitapatikana kabla ya chaguzi zinazofuata 2024/2025, juhudi za kuzuia uchaguzi huo usiwepo zitatumika kuuzuia.

Kauli hii imesikika kwa muda kitambo sasa, tokea ndani ya chama hicho; lakini kisichoelezwa ni jinsi gani adhma hiyo itatimizwa kwa ufanisi kamili, bila ya kuacha nyufa inazoweza CCM kuzitumia kujitangazia ushindi, hata baada ya uchaguzi wenyewe kuwa umevurugika kwa kiasi kiubwa.

Kuzuia uchaguzi siyo kazi nyepesi kuifanya; kwani mamluki wengi wapo ndani ya jamii yetu walio tayari kutumika kama maonyesho tu kuwa uchaguzi umefanyika.

Kuzuia uchaguzi kunahitaji mipango imara sana zinazoshirikisha wananchi wengi kuhakikisha kuwa uchaguzi hautafanyika.

Kwa kutangaza kuwa CHADEMA itazuia uchaguzi kuwepo, maana yake ni kwamba CCM wataitumia hali hiyo kuwazima CHADEMA kungali mapema, kwa kuwaweka ndani viongozi wanaosimamia zoezi hilo; na kusababisha juhudi yote kusambaratika.

Njia bora iliyo baki ni kwa CHADEMA kuadhimia kushiriki kwa nia kuu kabisa katika uchaguzi wowote utakaofanyika, na katika mazingira hata haya waliyozoea CCM kuyatumia kujitangaza washindi.

Inawapasa CHADEM kuzitambua njia zote zinazotumiwa na CCM katika uhujumu wa chaguzi hizo, na kuwa tayari kuwakabili CCM katika kila hatua ya kuhujumu uchaguzi huo.

Ni muhimu CHADEMA wawe wamejipanga vizuri zaidi kuliko nyakati nyingine zozote kuwakabili CCM katika uhalifu wao, tokea huko kwenye mitaa/mashina, hadi juu kabisa. CCM hufanya uhalifu, wanapovuruga taratibu za chaguzi. CHADEMA sasa wajipe kazi ya kuzuia uhalifu huo, na wananchi wataiona hiyo kazi na kuiunga mkono

CHADEMA wakijiandaa vizuri katika kila ngazi na hatua zote kama tulivyokwisha pendekeza humu JF mara kwa mara, uhalifu wa CCM utakomeshwa na wananchi wenyewe kwa kuongozwa na CHADEMA.

Ukitaka ufafanuzi wa mapendekezo tuliyokwisha wasilisha, tutaendelea kuyaweka humu. Lakini la muhimu zaidi, ni kwa kila mTanzania anayetaka mabadiliko ndani ya nchi hii, kutoa mapendekezo, anavyoona inafaa kuzuia uhalifu tunaofanyiwa na CCM kila wakati wa chaguzi.

Ni lazima tabia hii ikomeshwe na waTanzania wenyewe.
 
Ubunge na udiwani tumeona inawezekana kudhibiti CCM,

Tupe plan ya kudhibiti kura za Urais.
 
Ubunge na udiwani tumeona inawezekana kudhibiti CCM,

Tupe plan ya kudhibiti kura za Urais.
Njia ni zile zile, kuhakikisha kila kura ya mwananchi iliyopigwa haivurugwi na mtu yeyote yule.

Kwani kura za wabunge na madiwani zinatokea wapi mkuu Rabbon?
Hebu nikurudishie mpira huo ulionipasia mimi, eleza "ubunge na udiwani", inawezekana vipi kudhibiti, ambako kutakuwa ni tofauti na huko kwenye urais. Kura si ni hizo hizo zinazotokea huko huko, kwenye vituo vile vile?

Mwizi ukishambana mahala pamoja, hawezi akatoka hapo akaenda kuiba kwingine ambako ulizi ni ule ule.

CHADEMA wakikaza nati kwenye udiwani na ubunge, ni nati ile ile inayokazwa hata kwenye kura za urais.

Kwa hiyo kazi muhimu ni hiyo hiyo, ya kukaza nati kote kote.
 
Uchaguzi ujao utafanyika bila ya kuwepo Katiba mpya wala Tume huru ya Uchaguzi kwa maana ya Tume huru na Chadema itashiriki uchaguzi huo. Tuombe Mungu tu tufike salama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom