Kampeni za Uchaguzi zimeanza DRC, Fomu ya Urais Tsh. Milioni 150

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1700551977557.png

Wakati wagombea urais wa Tanzania wakitoa Sh5 milioni kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano, kwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wagombea urais wanatakiwa kuonyesha risiti ya malipo ya faranga za Congo milioni 160, sawa na zaidi ya Sh150.3 milioni kama ada zisizorejeshwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI).

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kiasi hicho kimepunguzwa kutoka dola 100,000 sawa na zaidi ya Sh250.5 milioni katika uchaguzi uliopita wa 2018.

Mpaka sasa wagombea 25 wameshajitokeza akiwamo Rais wa sasa Felix Tshisekedi akipambana na mpinzani wake wa karibu, Martin Fayulu ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2018 ilidaiwa alishinda ingawa si aliyetangazwa.
 
Imenivutia na km ikiwapendeza warudishe ule muamala wa mwanzo

Mgombea urais wa jamhur lazima awe sirias
 
Back
Top Bottom