Tetesi: Uchaguzi TCCIA Wa 07.11.2023 wadaiwa kuingia dosari za kujazia fomu kutokea ndani ya kamati ya uchaguzi na menejimenti

eagletai

New Member
Nov 1, 2023
1
0
Mimi Tai katika kupaa kwangu nimekutana na penyenye kuwa Uchaguzi wa TCCIA unaofanyika tarehe 07.11.2023 umeanza kupata dosari.

Viongozi wa Makao Makuu wameanza kupanga safu, ikiwa ni pamoja na kujazia fomu wagombea ambao hawakuomba nafasi hizo hadi zoezi linafungwa.

Penyenye hii inasema, kutoka chanzo kilicho ndani ya kamati husika kwa Mgombea mmoja kutoka mikoa ya Kanda ya Magharibi amejaziwa fomu, na kuonekana kuwa aliwasilisha fomu yake mtandaoni kabla ya kufungwa kwa zoezi la kujaza na kurudisha fomu mnamo tarehe 24.10.2023.

Kwa mtindo huu TCCIA itaendela kupoteza sifa ya kuwa Taasisi ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wenye Viwanda yenye nguvu na haiba nzuri na viongozi kupinduana kila kukicha, na au managementi kubadilishwa badilishwa kila mara.
 
Back
Top Bottom