Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,604
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kwa Maslahi ya Taifa, ambazo ni kuhusu jambo lolote la Kisiasa, Kiuchumi au Kijamii . Bandiko la leo ni bandiko muendelezo Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
Mabadiliko haya ya sheria yanaletwa katika mkutano wa Bunge hili, hivyo huu ni ushauri kwa Rais Samia na serikali yake, katika kubadili sheria ya uchaguzi, na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, nashauri jee tupige ndege wawili kwa jiwe moja?, au tuendelee kufanya chaguzi zetu kwa mazoea?
Ndege wa kwanza ni uchaguzi wa serikali za mitaa, usifanyike tena mwaka 2024 wala usisimamiwe tena na Tamisemi, na badala yake ufanyike mwaka 2025 pamoja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
Maendeleo ya kweli na maendeleo endelevu ni kukubali kubadilika kwa kwenda na wakati uliopo, tuache kufanya vitu kwa mazoea!
Tangu tumeanza kufanya chaguzi zetu, Tanzania tumekuwa tukifanya chaguzi mbili tofauti kwa muda tofauti, zikitumia sheria mbili tofauti na kusimamiwa na mamlaka mbili tofauti.
Chaguzi hizi ni uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi Mkuu, na husimamiwa na Tamisemi, huku ndiko madudu ya ajabu ya ukiukwaji wa demokrasia kuanzia.
Chama kinachoshinda serikali za mitaa, ndicho chama kinachokuja kushinda uchaguzi Mkuu unaofuata.
Ukiondoa chama kikubwa, na chama kikongwe CCM, vyama vingine vyote vya upinzani Tanzania ni vyama cha mtoto, viko too myopic havioni mbali, vinajikita kujipanga kwa nguvu kubwa kujiandaa kwa uchaguzi Mkuu wa 2025, kumbe mchezo haswa hufanywa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kwa vile Rais wetu Samia, ameonyesha nia njema ya dhati kwa mawazo, maneno na matendo, kuwatendea haki Watanzania, kwa kukubali kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, na kuunda Tume huru na Shirikishi ya u
Uchaguzi, Mnaonaje kama kwenye mabadiliko haya ya sheria yanayokuja, tutapiga ndege wawili kwa jiwe moja?.
Kwanza naendelea kusisitiza
kufanya mabadiliko ya sheria bila mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa, hivyo tunaipongeza serikali yetu kukubali kubadili sheria ya uchaguzi na kutupatia tume huru ya uchaguzi, ila nashauri tuanze kwanza mabadiliko ya katiba ndipo twende kwenye sheria!
Pendekezo la pili, ni tufanye uchaguzi wote kwa siku moja, na kusimamiwa na Tume moja huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar wanaweza kufanya chaguzi 5 kwa siku moja, Tanzania hatuwezi kushindwa kufanya chaguzi 4 kwa siku moja!. Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 halafu uchaguzi Mkuu 2025, kwa sasa tufanye mabadiliko ya katiba na sheria, halafu 2025 tufanye chaguzi zote 4 kwa siku moja, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa.
Kwa vile msingi mkuu na matatizo makuu ya uendeshaji wa siasa zetu yako kwenye katiba, katiba ndio kichwa cha yote na mengine yote ni kiwiliwili.
Kwa vile kuna mchakato wa katiba mpya utakaanza hivi karibuni, lakini kwa minaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na uchaguzi Mkuu wa 2025, tuanze na mabadiliko ya katiba hii hii iliyopo kwa kuibadilisha kwa hati ya dharura, ndipo tuje kwenye mabadiliko ya sheria za uchaguzi na kurekebisha Tume ya Uchaguzi tuunde Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
Bandiko hili ni bandiko
mwendelezo wa bandiko hili Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
Hitimisho,
Kwenye mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yanayotarajiwa kuletwa Bungeni kwa hati ya dharura kwenye mkutano huu, mnaonaje tukimshauri Rais Samia tupige ndege wawili kwa jiwe moja, kwa kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu kwa siku moja au tuendelee na mazoea?.
Naamini kabisa Rais Samia ana nia njema kuwatendea haki Watanzania, na rais msikivu akiongoza serikali yetu ni serikali sikivu.
Pia naomba kutoa angalizo la kitu kinachoitwa karma ambacho viongozi wetu hawakijui na matokeo ya kuidharau karma.
Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi Mkuu 2020, nilitoa ombi fulani humu jukwaani lenye kitu kiitwacho karmic consequencesOmbi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! kwenye bandiko hilo nilizungumzia karma ya nini kitatokea iwapo ushauri huo usipotekelezwa!, hivyo hata ikitokea ushauri huu nao ukapuuzwa kama ushauri ule, pia hakuna shida, mimi kwa upande wangu nitakuwa nimetimiza wajibu wangu.
Wasalaam.
Paskali