Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,505
- 113,620
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Makala ya leo ni kuhusu fursa ya kuufanya uchaguzi Mkuu ujao wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki.
Kwanza tukubaliane katika uendeshaji wa nchi, katiba, sheria, taratibu na kanuni ndio kila kitu.
Tangu tumepata uhuru wetu, nchi yetu Tanzania haijawahi kubahatika kupata rais ambaye ni mwanasheria, hivyo marais wetu wote wanawategemea wanasheria kwenye utengenezaji wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, hivyo kukitokea madudu ya ajabu ya kisheria kama ubatili kwenye katiba yetu, rais ambaye sio mwanasheria, hawezi kujua kwasababu anawategemea washauri wake ambao ni wanasheria.
Mtu ambaye sii mwanasheria, hawezi kuujua ubatili wa sheria, atawategemea washauri wake wamwambie kuhusu issues zozote za kikatiba na kisheria, ikitokea hao washauri nao japo ni wanasheria lakini hawajui sheria kikamilifu, ndio wanampotosha rais wetu, ndio maana bandiko hili ni utetezi kwa rais wa JMT Asilaumiwe kwa yanayotokea kwenye issues zote za katiba na sheria kwasababu yeye sio mwanasheria.
Japo kuna huu msemo wa Kiswahili usemao "Mkubwa ni jalala" na "aliyekutwa na ngozi ndiye aliyekula nyama" maadam rais ndio kipo chetu na macho yetu yote tumeyaelekeza kwake, lakini kuna mengine tutakuwa tunamuonea bure!, ndio maana niliwahi kushauri Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Mfano mzuri na mfano hai ni katiba ya Tanzania ya 1977, imenajisiwa kwa kuchomekewa kifungu fulani batili, waliokichomekea kifungu hicho ni Bunge la JMT, aliyeubaini ubatili huo ni Mahakama Kuu ya Tanzania, aliyeulinda ubatili huo ni Mahakama ya Rufani ya JMT, hivyo mpaka hapa ninapozungumza, usikute Rais wa JMT, she is an innocent victim, hajui kuwa katiba ya JMT imenajisiwa kwa ubatili fulani kwasababu wanasheria washauri wake rasmi ni ama hawaujui ubatili huo ama wanaojua lakini hawamwambii ukweli rais wetu, hivyo ikitokea tukaenda kwenye uchaguzi Mkuu wa 2025 bila kuuondoa ubatili huu, mtu wa kulaumiwa sio Rais Samia, kwasababu yeye sio mwanasheria, and after all, tumekuwa tukiendesha chaguzi zetu zote kwa ubatili huu, hivyo taifa letu kujikuta linalaanika kwa adhabu za karma bila kujijua!.
Kwenye ubatili huu ninao uzungumzia hapa, kiukweli kabisa mhimili wa Serikali, Bunge na Mahakama, umetukosea sana Watanzania!.
Katika mihimili hiyo mitatu, ni mhimili wa serikali tuu ndio pekee unapowakosea Watanzania, unaweza kuushitaki mahakamani lakini mhimili wa Bunge na mhimili wa Mahakama, unapowakosea Watanzania, hakuna mahali popote pa kuwashitaki zaidi ya kutegemea huruma ya rais wa JMT pekee. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Kama hao wanasheria manguli wabobezi na wabobevu wa sheria ambao rais wa JMT anawategemea wamshauri, ndio hao hao waliotunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, na wakaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria, sasa kunapotokea madudu ya ajabu ya marekebisho ya sheria kama haya yaliyoletwa jana Bungeni, unategemea nini?. Kumlaumu Rais Samia ambaye sii mwanasheria, ni kumuonea bure!.
Tukubali tukatae, Tanzania tuna tatizo kubwa la wanasheria wa ajabu!. Sakata la IGA ya DPW na Bandari ndio limetufungua macho!. Kwa mujibu wa katiba yetu Ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni batili!, lakini IGA hiyo, pamoja na ubatili wake wote, bado ilipitishwa na Bunge letu Tukufu hivyo hivyo ilivyo without any reservations!, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! tukauliza "IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii? mwisho wa siku hii IGA, iliwekwa pembeni HGA safi ikasainiwa. Sasa unapowategemea wanasheria wa type hii ndio washauri wa sheria na wasaidizi wa Rais Samia, unategemea nini?!. Tusimlaumu kabisa Rais Samia.
Unaweza kufuatilia baadhi ya madudu ya ajabu ya kisheria yaliyofanywa na wanasheria wetu!
Mpaka leo ninapoandika hapa, ubatili huo bado uko ndani ya katiba yetu!. Kwa vile Rais wa JMT sio mwanasheria, tulichofanya akina sisi, ni kumweleza Rais Samia kuwa baadhi ya wanasheria anaowategemea hawamsaidii, hivyo akina sisi tukajitolea kuwa bypass and reach out kumfikia Samia mwenyewe na kumweleza kupitia mitandao ya kijamii na makala magazetini kuwa katiba yetu ni batili!.
Kuhusu huu ubatili kwenye katiba yetu, kama ni kumweleza Rais Samia, tumemweleza sana!.
Kikosi kazi kilipomaliza kazi tumampongeza tukamkumbusha. Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
Wakati hayo yote yakiendelea, tukamsikia Rais Samia akizungumzia haki tukajiuliza Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
Kisha watu tukajitolea kufanya uelimishaji umma kuhusu katiba kupitia vipindi vya TV, Redio, makala magazetini na kwenye mitandao ya kijamii.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=ElCUzq4FKy4oiGxP
Nikazungumza na wanasisa mbalimbali wana mategemeo gani kuhusu hali ya siasa, nikatengeneza Vox Populi, kwenye Vox Populi, ukikusanya sauti za wengi, ukaziweka sauti hizo pamoja, sauti hizo haziwi tena ni Vox Populi, zinageuka ni Vox Dei!.
Baada ya Serikali yetu sikivu kukubali italeta mabadiliko ya sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya tume ya uchaguzi, tukashauri tena na tena!. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
Hatimaye jana Ijumaa, hiki ndio tukaletewa!. Sisi wa kupongeza tukapongeza Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii
Kuna watu watamlaumu Rais Samia kwa kuamini ni yeye!, kumbe masikini ya Mungu, sio Rais Samia, yeye sio mwanasheria, hiki kilicholetwa Bungeni jana yaani ile Miswada ni kazi ya washauri wake ambao ni wanasheria. Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
Sasa kwa vile tunayo miezi 3, ya kujadili na kutoa mapendekezo yetu, nashauri na kuwasisitiza tusimlaumu Rais Samia, wala tusiwalaumu wasaidizi wake, bali tutoe mapendekezo yetu kama tulivyofanya kwenye ile IGA, tukapata HGA nzuri.
Tupendekeze sheria nzuri ya uchaguzi na Tume huru na Shirikishi ya uchaguzi, naamini kabisa Rais Samia ni Rais msikivu na tutasikilizwa na mwisho wa siku tutabadili kwanza katiba kuondoa ubatili, kisha tutaunda Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, Tutabadili sheria yetu ya uchaguzi kuleta sheria mzuri ya haki ya uchaguzi ambayo itasawazisha uwanja wa siasa, a level playing field, tutafanya uchaguzi wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa, hivyo utafanyika kwa siku moja na utasimamiwa na Tume moja Huru ya Uchaguzi na uchaguzi Mkuu wa 2025 utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki!.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali

Haya kama haitoshi, baada ya serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria batili kutungwa kuwa sheria, Bunge letu limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, kuanzia Katibu wa Bunge ni mwanasheria nguli mbobezi na mbobevu, mwanasheria mkuu wa serikali ni mwanasheria nguli mbobezi na mbobevu, Waziri wa sheria ni mwanasheria nguli mbobezi na mbobevu, Katibu Mkuu Wizara ya sheria ni mwanasheria mbobezi na mbobevu, na ndani ya Bunge kuna wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, wakiwemo hadi wanasheria wahitimu wa Yale na Harvard University ambavyo ndio top of the top duniani kwa vyuo vya sheria, wote hawa hawakuona huo ubatili kwenye miswada hiyo, hivyo Bunge letu Tukufu likatunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, na kumpelekea rais akaisaini kuwa sheria!. Kwa rais wa JMT kusaini sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba na kuwa sheria!, huku ni kwenda kinyume cha Ibara ya 56 A ya katiba yetu!, lakini rais wetu hatuwezi kumlaumu kwa kusaini sheria hiyo kwasababu rais wa JMT sio mwanasheria, kama wasaidizi wake ambao ni wanasheria manguli wabobezi na wabobevu hakuuona ubatili huo, yeye rais ambaye sio mwanasheria anategemewa angefanya nini zaidi ya kuisaini, sasa rais anaposaini sheria batili ianze kutumika, wakulaumiwa kwa ubatili huo sio rais aliyesaini bali ni wasaidizi wake wanasheria waliompelekea!, hivyo rais wa JMT hapaswi kulaumiwa!. Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
Akatokea Mtanzania mmoja mzalendo wa kweli wa taifa hili, akaubaini huo ubatili, akafungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania, Mahakama ikatamka huo ni ubatili, kinachobatilisha sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, ni katiba yenyewe na sio Mahakama!, kazi ya Mahakama ni kuutamka tuu huo ubatili, lakini anayebatilisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT ni katiba yenyewe!. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
Sasa kitu cha ajabu kabisa kuhusu serikali yetu, hata baada ya Mahakama Kuu kutamka huo ubatili, serikali yetu ya wakati huo, ikafanya jambo la ajabu sana!. Ikapeleka Bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, na kuuchukua ule ubatili na kuuchomekea ndani ya katiba yetu kiubatili, hivyo sasa ubatili huo, ukawa uko ndani ya katiba!.
Hawa ni wanasheria wa aina gani ambao Mahakama Kuu imetamka kipengele fulani ni batili kwasababu kinakwenda kinyume cha katiba, kisha unauchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya katiba yetu ili kuuhalalisha!.
Mzalendo yule hakubali katiba yetu inajisiwe kwa kuchomekewa ubatili, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi, ikatangaza mabadiliko hayo ya katiba ni batili na yamechomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili!.
Serikali yetu ndipo ikatoa kubwa kuliko kwa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kuwa Mahakama Kuu haina mamlaka kutengua kipengele cha katiba kilichochomekewa na Bunge ndani ya katiba kiubatili hata kama kipengele hicho ni batili, mamlaka pekee yenye uwezo wa kuuondoa ubatili huo ni Bunge lenyewe, hivyo Bunge likaamriwa kuuondoa ubatili huo!.
Mpaka leo ninapoandika hapa, ubatili huo bado uko ndani ya katiba yetu!. Kwa vile Rais wa JMT sio mwanasheria, tulichofanya akina sisi, ni kumweleza Rais Samia kuwa baadhi ya wanasheria anaowategemea hawamsaidii, hivyo akina sisi tukajitolea kuwa bypass and reach out kumfikia Samia mwenyewe na kumweleza kupitia mitandao ya kijamii na makala magazetini kuwa katiba yetu ni batili!.
Kuhusu huu ubatili kwenye katiba yetu, kama ni kumweleza Rais Samia, tumemweleza sana!.
Hapa ni baadhi ya sheria hizo
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
- Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
- Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Bandiko hili ni utangulizi wa mabandiko haya
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
- Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo
- Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
Kikosi kazi kilipomaliza kazi tumampongeza tukamkumbusha. Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
Wakati hayo yote yakiendelea, tukamsikia Rais Samia akizungumzia haki tukajiuliza Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
Kisha watu tukajitolea kufanya uelimishaji umma kuhusu katiba kupitia vipindi vya TV, Redio, makala magazetini na kwenye mitandao ya kijamii.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=ElCUzq4FKy4oiGxP
Nikazungumza na wanasisa mbalimbali wana mategemeo gani kuhusu hali ya siasa, nikatengeneza Vox Populi, kwenye Vox Populi, ukikusanya sauti za wengi, ukaziweka sauti hizo pamoja, sauti hizo haziwi tena ni Vox Populi, zinageuka ni Vox Dei!.
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=vi_1SU4oPZNEM6in
View: https://youtu.be/YLjwcGPwzO8?si=lgGyYMJevslePh_O
View: https://youtu.be/5kIid09GCqQ?si=e_VHKL6MDAMUtQAC
View: https://youtu.be/cHxuVN8njWM?si=XjFNqdA8Nz6Pzu9b
View: https://youtu.be/U2sP1sh3Si8?si=2abRyuQAzpkRzvys
View: https://youtu.be/L1VfloknySk?si=miWO1dPE1JHb-zef
View: https://youtu.be/4xNWWz3kNLg?si=2NrPRsdPJSPav_jX
View: https://youtu.be/2Iw3KXte-2c?si=JTkvEC_FkUcJ0AqZ
View: https://youtu.be/Li8Yu29CwV4?si=N_u0Usl9KlJkHQW7
View: https://youtu.be/h3TFKlNHV98?si=szfhnQ0sUvluEXTy
View: https://youtu.be/yy8bq2PnZwc?si=Jx5eQ5NHfPRGcTk5
View: https://youtu.be/dtb2ut-bGdU?si=PB2o8WQUVUumxI6O
View: https://youtu.be/w0WiYIr1t90?si=93tUW_cULpmE0vl5