ABUBAKAR Salum ‘Sure Boy’. Fundi mmoja wa mpira kuwahi kutokea nchini. Sio huyu wa sasa anayecheza pale Yanga, hapana, huyu ni baba yake mzazi. Ndiye mwenye jina halisi la Sure Boy.
Alipewa jina hilo kutokana na kazi yake njema uwanjani. Alikuwa na kasi kubwa uwanjani. Akipiga krosi na pasi...