Nov 25, 2023 11:03 UTC
- Netanyahu na mawaziri wakuu wa Uhispania na Ubelgiji
Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen, imesema katika taarifa yake kwamba waziri huyo amewaita mabalozi wa Uhispania na Ubelgiji kufanya "mazungumzo ya kukemea," akilaani kile alichokitaja kuwa madai ya uwongo ya Mawaziri Wakuu wa Uhispania na Ubelgiji ambayo amesema yanaunga mkono ugaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania, Jose Manuel Albares amejibu madai hayo ya Israel na kutangaza kupitia televisheni ya taifa jana jioni, Ijumaa, kwamba amemwita balozi wa Israel mjini Madrid ili kutoa ufafanuzi wa shutuma za serikali ya Tel Aviv, ambazo amezitaja kuwa "uongo na zisizokubalika."
Ameongeza kuwa: "Suluhisho la sasa la mgogoro wa Gaza halitoshi," na kusisitiza kwamba Israel lazima iwe ya kwanza kuchukua "mkakati wa kina" wa kutatua mzozo wa Israel na Palestina, ikiwa ni pamoja na Ukingo wa Magharibi na Quds Mashariki.
Waziri Mkuu wa Uhispania pia ameitaka jamii ya kimataifa na Israel kutambua rasmi taifa la Palestina.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ubelgiji amesisitiza kuwa Israel lazima iheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na kwamba "mauaji ya raia lazima yakome