Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Mfumo wetu wa nchi kiongozi ni mfalme na yeyote atakayenyanyua mdomo atachukuliwa hatua. Mfumo wa majeshi ndiyo mbaya kabisa kwa sababu wanaamini kwamba wapo juu ya kila jambo.
Dr. Makakala ni kiongozi wa taasisi ya usalama nchini anayepitia magumu kutoka kwa wale wanaotamani aondolewe kwenye nafasi yake.
Amekutana na matusi ya kila aina lakini hakuna siku amewahi kusikika adharani akipambana na wananchi
Ni kiongozi pekee aliyebaki kwenye taasisi za kijeshi ambaye aliteuliwa na Magu. Pamoja na nguvu kubwa iliyokuwa inatumika na vitisho wakati wa JPM lakini huyu mama hakuna Sehemu kuna sauti yake akielekeza mtu kuadhibiwa. Miaka yote amekuwa kimya na hii naamini ndiyo sababu Mhe. Rais wa sasa hakuona umuhimu wa kumtoa au kumpangia kazi nyingine.
Mimi nimetembea Duniani na mara kadhaa nasema hapa kuwa Uhamiaji ya kabla ya Makakala ilikuwa imeoza. Leo hii hakuna fedha ya serikali isiyolipwa uhamiaji kwa control number, hakuna huduma ambayo wamejificha nayo ofisini bali huduma zao zote wanazitoa mtandaoni kupitia www.immigration.go.tz tofauti na awali.
Visa online zimesaidia sana kwenye support ya royal tour, hakuna mtalii aliyelalamikia huduma zetu pamoja na ujio wa wageni wengi. Kipindi cha COVID nakumbuka huyu mama aliweza kutumia sana hekima wageni wakaendelea kuwepo nchini hata baada ya visa zao kuisha. Kwa tuliokuwa na connection ya wageni that time tutakuwa mashahidi. Mimi kuna wageni nilikuwa nakaa nao kwangu wameishiwa lakini sikuwahi kulipia huduma ya ziada badala ya kwenda Mweza kuwaongezea muda and that time kumbuka alikuwepo JPM. Nimejifunza mengi sana kwa reform za huyu mama
Ninapoona mMadeleka anamtusi kila siku napata wasiwasi may be wapo watu nyuma ya madeleka wanataka kupewa hii nafasi? Wakipewa wataweza kwenda na kasi hizi au watarudisha Idara hii kule tulipotoka?
Lakini hata kama wanataka nao wapewe hii nafasi wanaamini Madeleka ni mtu sahihi wa kupush agenda zao. Wakati mwingine najiuliza Makakala anawanyima familia ya Madeleka msosi ? Mwisho, najiuliza Madeleka kubishana na mtu asiyejibu na anayeendelea kuchanja mbuga siyo ishara tosha kwamba amedharauliwa?
Hakuna nishani inayotolewa kwa wingi wa matusi na Majungu. Mwacheni mama wa watu atembelee V8 hadi siku aliyemteua atakapoona ametosheka na usaidizi wake. Hao wanaoalalamika vyeo vimetolewa kwa upendeleo naamini ndio hao hao waliomtuma Madeleka. Yawezekana walishajipanga wapande juu wenzao wakaona nia yao mbovu na sasa wamepandisha wenye nidhamu........Kwa sisi tuliopita jeshini miaka 1990 hakuna kulalamika wala kugoma , ikibainika unarejeshwa uraiani ukawe mwanasiasa.
Makakala chapa kazi kwanza ukujiteua mwenyewe uliteuliwa na Mhe. Rais. Endelea kuwapuuza hao wanaokuchafua huku ukimtegemea Mungu katika kazi na maisha binafsi.