Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waliotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda
Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.
Akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alitangazwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?
Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilichokuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani