Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Hii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.

Mi nipo zangu home jana inaingia simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.

Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.

Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.

Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.

Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.

Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.

Mimi walienda kusema nafuja sana pesa badala ya kuwasomesha watoto wao. Mtu kazaa watoto 13 anataka nimsomeshee... Mimi nina 3 tu. Bado wanaenda kusema nakuaje na watoto wachache ... Mwanaume gani. Mke amenikalia kichwani anarudi jioni kama mwanaume. Wanataka wife awafulie nguo zao. Na wanakuwa wakali akirudi awapatie chakula n.k sina hamu na ndugu kabisa.

Mmoja tumekaa naye mwaka mmoja amekuja nimsomeshe diploma. Akirudi toka chuo anaangalia TV mpaka saa 4 akipewa kazi basi za home siku yupo asaidie... Anasema anateswa sana hawezi soma. Nikasubiri likizo. Akaenda kwao kusalimia. Nikamwambia atafute chuo aendelee kusoma huko, nitamlipia ada.

Alilia sana anataka arudi Dar. Nilimwambia huku wifi yako atakutesa hutapata muda wa kusoma. Akabembeleza sana nilimkatalia coz alishanipakaza sana kijijini na kumchafua sana wife. Na mtu mwenyewe ni ndugu wa mbali kabisa..

HAWA WAGENI WENGINE NDO HUNAJISI WATOTO NA UNDUGU UNAISHIA HAPO HAPO. MNAHARIBIANA FUTURE. KILA MTU AKAE KWAKE. DUNIA YA SASA IMANI IMEKWISHA. TUSAIDIANE KATIKA SHIDA LAKINI SI KUVAMIANA TU NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA UKARIMU. NDUGU WENYEWE IMANI IMEWATOKA. ANGALIA WANAOBAKWA, NAJISIWA AU LAWITIWA. MHUSIKA UTAKUTA BABA, BAMDOGO, MJOMBA, COUSIN NA JIRANI KWA MBALI KIDOGO.
 
Mtu atoe taarifa ujipange, usipotoa taarifa nitakuacha kenye mataa

Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.
 
Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.
Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k
Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.
Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!
Kwendreni huko.
Jamaa mbona una hasira dhidi ya ndugu zako, wallikufanya nini mpaka unawaitia Mijitu?

Mkuu Jaribu kuwa Mnyenyekevu basi.

Hao unaowadharau ipo siku utawakumbuka na hutawaona.

Kama huwezi kumsaidia mtu basi achana naye ila usimpe majina mabaya eti Mijitu.....Itakuwa wewe Kweli Umeolewa maana hizo hasira tu sio kidogo.
 
Mkifa mitoto yenu inarudi mikoani kunyanyaswa......ndugu mliowaita wanoko hamuwataki wanachukua Mali zote ulizochuma....mke wa marehemu akishtaki, ndugu hutumia pesa za marehemu kushinda kesi....Hapo marehemu umelala kimya kaburini. Hii ndiyo dunia mkuu
 
Jam

Jamaa mbona una hasira dhidi ya ndugu zako wallikufanya nini mpaka unawaitia Mijitu?

Mkuu Jaribu kuwa Mnyenyekevu basi.

Hao unaowadharau ipo siku utawakumbuka na hutawaona.

Kama huwezi kumsaidia mtu basi achana naye ila usimpe majina mabaya eti Mijitu.....Itakuwa wewe Kweli Umeolewa maana hizo hasira tu sio kidogo.
Bush Dokta nakuheshimu Sana.
 
Mkifa mitoto yenu inarudi mikoani kunyanyaswa......ndugu mliowaita wanoko hamuwataki wanachukua Mali zote ulizochuma....mke wa marehemu akishtaki,ndugu hutumia pesa za marehemu kushinda kesi....Hapo marehemu umelala kimya kaburini.Hii ndiyo dunia mkuu
Tuwe wanyenyekevu tunapopata mafaniko tusione wengine ni takataka hawafai.
Ukifa ndio watamfariji mkeo na watoto wako
 
Ni sahihi ila lazima uwajue vizuri ndugu zako mapungufu yao, kama unaweza kusaidia, just relax na msaidie..... Ni kweli hapa mjini sometimes tunapokwenda huko kijijini tunajitapa na kuonekana tunamaisha safi na tumeyapatia kumbe naishi stoo, yaani chumba kimoja tu kila kitu hapo, sasa anapokuja yule uliyemlisha maneno na kujua kwa yale aliyoniambia hata nikimfanyia surprise haina noma, kumbe tunamaisha magumu yasiyopimika. Nadhani tuweni tu wanyenyekevu na kupunguza kuongea sana tunapokwenda vijijini kwetu.
 
Mi nipo zangu home jana inaingiza simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.
Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za simu za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
 
Kiukweli kwa maisha tuliyo nayo sasa inapendeza mgeni akija aje kwa taarifa.

Ni asiyeelewa tu namna dunia imefikia wapi kwa sasa ndo ataona ye mgeni akija tu kwake bila taarifa ni sawa.

Hawa hawa tunaowaamini wengi wamekuwa mwiba kwa baadhi ya familia hasa baada ya kuja bila kuwa na vya msingi vilivyowaleta.
 
Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
Kama ni MwanaJF na akajua umekuja kumsema mtandaoni itakuwaje?
 
Hii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.

Mi nipo zangu home jana inaingiza simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.

Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.

Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.

Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.

Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.
Nanyie muache upimbi wa kutuambia tukija Dar tuwatafute. Nguchiro nyie
 
Back
Top Bottom