Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.
Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.
Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.
Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
CHADEMA wanatengeneza maneno kuwa CCM inamuogopa Mhe. Mbowe na CHADEMA ndio maana anapingwa asigombee tena.
Hii si kweli na ni upotoshaji mkubwa sana, chama chenye wasomi, wataalamu na manguli wa siasa Tanzania kiogope chama ambazo hakina mbadala zaidi ya ‘DJ’?
Toka kuanzishwa kwa CHADEMA...
Sijawahi kuipenda CCM toka nimepata uelewa wa vitu. Mwanzoni kabisa nilikua naipenda CUF, ila katika miaka ya 2005-2010 siasa za Zitto pamoja na Dk. Slaa zilinivutia sana eventually nikajikuta nasupport CHADEMA. Miaka kadhaa ikapita Zitto akafukuzwa chama kwa maneno mengi sana kama in sellout na...
Frederick Sumaye ameita waandishi wa habari leo Jumatano Desemba 4, 2019.
Sumaye ameitisha mkutano huo siku chache baada ya kushindwa uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.
Licha ya kuwa mgombea pekee, alipigiwa kura 48 za hapana kati ya kura 76.
Kulingana na taratibu za chama hicho...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa kuona mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akitumia nembo ya taifa katika barua yake ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika leo katika jengo la LAPF, lililopo Kijitonyama...
WanaJF,
Ni kipindi kingine muhimu kwa mustakabali wa siasa za Tanzania. Uchaguzi mkuu wa Chadema sio tu kwamba ni uchaguzi wa kawaida bali ni uchaguzi wa chama kikuu na tishio kwa chama tawala.
Baada ya kumaliza kuwapata viongozi wakuu wa chama nafasi nyingine muhimu inayotizamwa na wengi ni...
Ni kiherehere changu tu kujiuliza swali la kimsingi kabisa la demokrasia ndani ya CHADEMA. Mimi si mwanachama wa chama hiki cha upinzani lakini ndio chama rasmi kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni.
Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro...
WanaJF,
Nchi iko katika heka heka kubwa kutokana na chama kikuu cha upinzani CHADEMA kuendelea kufanya uchaguzi wake katika ngazi ya Kanda.
Kwa idadi kubwa Watanzania wanafuatilia kwa karibu sana uchaguzi huu pengine kuliko ule uchaguzi wa serikali za mitaa uluosusiwa na upinzani.
Kwa...
Wananchi wanapenda mabadiliko sana ila vyama vinavyojiita vya upinzani Nchini hususani Chadema kimekuwa kikizorotesha sana uhai upinzani.
Ushahidi wa haya unayoyasema upo wazi kabisa:-
1. CHADEMA ndiyo waliomkera Dr Wilbroad Slaa kiongozi ambaye alipaswa kuzalisha vijana wengi kwa...
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi amesema anafuatilia kwa makini sana uchaguzi wa viongozi wa CHADEMA kuhakikisha katiba inafuatwa na haki inatendeka kwa wagombea wote.
Msajili amesema endapo katiba itakiukwa kwa makusudi basi uongozi utakaochaguliwa utakuwa ni batili na...
Hatimaye Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mh Mbowe amerudisha fomu za maombi ya kuendelea kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano.
Kadhalika Waziri Mkuu Mstaafu aliyejiwekea historia ya kukaa madarakani kwa miaka 10 mfululizo bila kutumbuliwa Mzee Sumaye naye amerudisha fomu huku...
Wanabodi,
Hili ni bandiko la maswali yenye facts
Jee kuna ubishi kuwa Upinzani Tanzania Unamatatizo?. Ni matatizo gani na usaidiweje?.
Vyama vingi vya Upinzani Havina Succession Plan, kwanini vyama hivyo havina succession plan na sio tuu kwenye uongozi wa ndani, hata kwenye ubunge na udiwani...
Mwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.
Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha...
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha.
Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania...
Nimetaarifiwa na kada mkongwe wa CCM aliyeko Zanzibar kuwa mwezi wa December 2019 madiwani zaidi ya 100 wa Chadema na ACT wazalendo watahamia CCM katika kuunga mkono juhudi za mh Rais Magufuli.
Inaelezwa kuwa Chadema itapoteza halmashauri zote inazoziongoza zikiwemo zile za majiji, manispaa na...
Acha wale watano waliounga juhudi leo kuna namba kubwa zaidi tena ikitarajiwa kuamua kwa pamoja kurejea CCM muda wowote kuanzia kesho.
Duru zinatabanaisha maombi ya madiwani hao yapo mezani yakifanyikiwa kazi na Ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha na hata wangeruhusiwa leo kufanya hivyo wangefanya...
Leo huko jijini Arusha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mh. Freeman Mbowe amerejesha fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani CHADEMA.
Mh Mbowe amerejesha fomu hiyo aliyochangiwa na kuchukuliwa na vijana wa chama chake yenye thamani ya 1 million kwa Katibu wa chama hicho...
Wanachama wengi wa chadema wanamwangalia mbowe kwenye mazuri aliyofanya tu bila kuangalia sehemu alikoshindwa kama
1: Kushindwa kuchukua hatua kali za kichama kupinga kuzuiwa kwa mikutano na mahandamano ya vyama vya siasa.
2: Kutokuwa na ofisi za kujenga majengo mengi wanapanga nilitegemea...
WanaJF
Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.
Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman...
Wasalaam, wahenga wana msemo kwamba usipookoboa utaula wa chuya.
Kufuatia wimbi la viongozi mbalimbali wa CHADEMA kutimkia CCM (hasa wale waliohamia kutoka CCM) wana CHADEMA asili wamejenga hofu ya kutowaamini viongozi wote waliosalia ndani ya CHADEMA ambao walihamia kutoka CCM.
Hapo juzi...