Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA atakuwa kati ya hawa...

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF,

Ni kipindi kingine muhimu kwa mustakabali wa siasa za Tanzania. Uchaguzi mkuu wa Chadema sio tu kwamba ni uchaguzi wa kawaida bali ni uchaguzi wa chama kikuu na tishio kwa chama tawala.

Baada ya kumaliza kuwapata viongozi wakuu wa chama nafasi nyingine muhimu inayotizamwa na wengi ni nafasi ya Mtendaji mkuu wa chama yaani Katibu Mkuu.

Kwa sasa yanatajwa majina mengi yanayoweza kuchukua hiyo nafasi muhimu sana. Ila kwa asilimia kubwa Katibu Mkuu mpya anatarajiwa kuwa mmojawapo kati ya hawa wafuatao:

- John Mnyika
- .Salum Mwalimu
- John Heche

Kwa kadiri tutakavyokaribia vikao vikuu vya uchaguzi tutawaletea wasifu wa kila mmoja kwa hawa wanaodhaniwa kumrithi Katibu Mkuu anayemaliza muda wake.

Updates Alfajiri saa 11 - 20.12.2019

Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa chama Taifa amemteua John John Mnyika kuwa Katibu Mkuu Chadema

Pia Mbowe amewateua Benson Kigaila kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Katika uteuzi mwingine Kiongozi huyo mkuu wa Chadema amemteua John Heche kuwa mjumbe wa Kamati Kuu

Baraza Kuu kwa kauli moja limeridhia uteuzi huu wa Mwenyekiti wa chama na shangwe zimetawala katika ukumbi huu wa Mlimani city.
 
Hawa wote nafikiri wana kesi. Tuombee kwanza wapone kule ndipo tube kwenye hii hoja but Kwangu wote wazuri. Navutiwa na Heche vile anavyotamba Bungeni. Ni mwasilishaji mzuri sana wa hoja. Mnyika ana nafasi yake kubwa tu.
 
Back
Top Bottom