CHADEMA haiwezi kwenda Ikulu - Prof. Safari

Leo umefufuka enh. Ngoja nikurudishe kuzimu kabla hujatupasua vichwa humu.

Kwanza pitia huu uzi, ukapate kazi ya kujitibu PRESHA, posho za 7,500/= zitawaua.
 
..amesema lazima kuwepo na TUME HURU YA UCHAGUZI.

..pia ameeleza jinsi CCM walivyomdhulumu na kumharibia career, ndoto, na mipango yake ya kwenda kufanya kazi International Court of Justice, yenye makao makuu The Hague.
 
JokaKuu, 6:25 "....kama ukisoma magazeti haya kuhusiana na mheshimiwa Sumaye na nini, na huyu Cecil Mwambe; unaona kwamba watu wakitaka kugombea na nini....inaweza kuonekana kama loose talk, lakini tusichukulie kirahisi rahisi kiasi kile. Then ni kwamba tufanyie kazi. Kama watu wanalalamika tusinanhii, sio kama jongoo unalitupia pembeni, hapana lazima kufanyia kazi vitu kama vile, hapa tusidharau..." Prof. Safari.
 
"Tusichukulie kama loose talk,tusidharau"

Pamoja na kuzungumza mengi kwa busara ila hilo la Mwambe na Sumaye namna magazeti yanavyoandika,jibu ndiyo hilo🖕🏿
 
Hayo yote ye wala hajaona
Na hii hujasikia (yaani umetia pamba masikioni):-
6:25 "....kama ukisoma magazeti haya kuhusiana na mheshimiwa Sumaye na nini, na huyu Cecil Mwambe; unaona kwamba watu wakitaka kugombea na nini....inaweza kuonekana kama loose talk, lakini tusichukulie kirahisi rahisi kiasi kile. Then ni kwamba tufanyie kazi. Kama watu wanalalamika tusinanhii, sio kama jongoo unalitupia pembeni, hapana lazima kufanyia kazi vitu kama vile, hapa tusidharau..." Prof. Safari.
 
Nimeanza kuamini kuwa wangwe walimpiga vita baada ya kuweka nia ya kugombea.

Mbowe ni mtu hatari kuliko hatari yenyewe.

Serikali iwe macho sana na huyo Mbowe.

Hata umaarufu wa Lisu huenda ulitiliwa mashaka na Mbowe.
Kwa nini ampe umakamu wa mwenyekti na sio Mwenyekiti?
 
Acha kudanganya.. juzi si tumekutana getini wote tukotoka kuunga juhudi?
 
Ametumia haki yake ya kikatiba. Ila ukiwaza kwa makini utajua kuwa kuingia ikulu bila tume huru ya uchaguzi inawezekana kwa nguvu ya ziada kutumika. Hata wazungu waliachia nchi yetu wakiwa na katiba yao hiyo hiyo na Nyerere akawa waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika kwa katiba ya mkoloni.Kwa hali ya kawaida tume huru haipo pasipo madiliko ya katiba kwasababu muundo wa tume katiba imeelekeza.

Na katiba mwenye maamuzi ibadilishwe ni rais na ndiye mwenyekiti wa ccm. Professor aliwaza hili kuwa sio rahisi kupata tume aliyoshauri au yeye aliweka njia gani ya kupata hiyo time huru bila ccm kuathiri maslahi yao kwenye tume ya leo?. Mi nasema kuitoa ccm ni rahisi sana ila wenye nafasi za juu za chadema wamezidisha mno hekima. Yaani kwa katiba hii hii ccm wanawezekana kutoka tu. Kama walivyotoka wazungu wakiwa na katiba yao mkononi.
 
Back
Top Bottom