Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
343
Points
1,000

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined Apr 18, 2017
343 1,000
Frederick Sumaye ameita waandishi wa habari leo Jumatano Desemba 4, 2019.

Sumaye ameitisha mkutano huo siku chache baada ya kushindwa uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Licha ya kuwa mgombea pekee, alipigiwa kura 48 za hapana kati ya kura 76.

Kulingana na taratibu za chama hicho uchaguzi huo utarudiwa.

Taarifa iliyotolewa na Evanuru Nasari, katibu msaidizi wa ofisi ya Waziri Mkuu huyo mstaafu inaeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia masuala ya siasa nchini na mwenendo wa uchaguzi unaoendelea CHADEMA.

Nipo hapa Kisenga kuwajuza kile kitakachojiri.

Stay tuned

======


UPDATES:1105HRS

Sumaye.PNGHOTUBA YA SUMAYE
Naomba tangazo lililotoka jana mliache kama lilivyo, Naomba radhi.Kuna mambo mengi yameandikwa juu ya kikao hiki, watu wanapiga ramli, Myapuuze.

Agost 2015 nilieleza kwanini nahamia upinzani, sababu kubwa ilikuwa kuimarisha Demokrasia ya Ushindani na vyama viwe na nguvu zinazofanana. Nlieleza wazi kuwa sihami sababu ya chuki yoyote wala na CCM. Nilisema nahamia upinzani ili kuupa upinzani nguvu, na hili litakuwa na manufaa kwa CCM sababu hawatalala usingizi

Leo CCM hawalali usingizi sababu ya uchaguzi wa 2015. Chama chochote kisipolala usingizi, kikafanya kazi ipasavyo wanaonufaika ni Wananchi.

Nilijiunga CHADEMA Novemba 2015 na ninaamini mchango wangu ulikuwa mkubwa. Simaanishi CHADEMA ilikuwa dhaifu bali imepata nguvu baada ya watu kuhamia 2015.

Sikuja CHADEMA kutafuta vyeo, nimehamia CHADEMA wakati wagombea walishateuliwa. Urais alikuwa kapewa Lowassa na Duni Hadji. Nlikuja upinzani ili tuwe na vyama vyenye nguvu sawa wa kuwania uongozi wa dola.

Nilisema hata CHADEMA ikishinda na kuchukua dola ising'ang'anie. Nliwaambia wawe tayari kuwasilikiliza wananchi pindi wasipochaguliwa.

Natamani kuwe na Demokrasia ya kweli kuanzia ndani ya vyama vyetu. Natamani vyama visikae madarakani kipindi kirefu sana ili wananchi wanafaike.

Nlipojiunga CHADEMA nilipokelewa vizuri, wananchi wakaniomba nigombee Kanda ya Pwani nikakubali.

Kujiunga kwenye upinzani sio jambo lahisi na kunahitaji moyo. Japo nilieleza ni kwa nia njema, nilianza kupata misukosuko, mashamba yalichukuliwa, huduma zangu zilipunguzwa kuliko wastaafu wengine, familia yangu ilianza kupata mateso. Nilivumilia sana na familia yangu ilianza kuzoea na hatukua tunagombana tena.

Watu walinifuata wakanichukulia fomu ya kugombea uwenyekiti Pwani. Wakanichukulia fomu nikagombea. Nongwa ilikuja nilipotaka kugombea uenyekiti wa chama Taifa. Nilitaka kuondoa hisia za hakuna Demokrasia ndani ya chama na nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA hauguswi ndio maana nikachukua fomu, kumbe nilifikiri vibaya.

Pamoja na hayo yote hata kama tungetaka kumlinda Mbowe wetu, wangetumia njia sahihi. Wajumbe walionichukulia fomu ndio hao waliofanya mpango wa kuninyima kura kwa kupewa hela na kupigiwa simu. Kwanini hawakuniambia mapema. Nafasi ya Kanda haihusiki na uchaguzi wa Taifa.

Kabla ya uchaguzi haujaanza nilitahadharisha kwamba mlichopanga sio sahihi. Kama mkipiga kura kama mlivyopanga, mtakuwa mmeudhihirishia umma kwamba nafasi ya Mbowe haiguswi. Walidhani wananikomoa mimi bali wameharibu Taswira ya chama. Mbowe, hao watu wa cabinet yako wanakudanganya.

Nasitisha rasmi kugombea nafasi ya Uenyekiti. Kwa Usalama wangu. Tulipokuwa Arusha Mbowe alituambia Sumu haionjwi kwa kuilamba nami sitaki kuilamba.

Ndugu yangu Mbowe najua utakuwa mwenyekiti wa chama, ondoa hayo makundi. Prof. Safari alitoa ushauri akaambulia matusi, hata mimi najua nitaambulia matusi.

Kwa kitendo hiki kilichotengenezwa na viongozi wa juu wa CHADEMA, nimefedheheka sana. Eti nimekosa adabu kwa kugombea Uenyekiti wa CHADEMA. Kwa haya matendo, akuchukiae hakuambii toka.

Najiondoa CHADEMA kuanzia leo na sijiungi na chama cha siasa kingine. Nitatumika kutoa ushauri watakaponihitaji chama chochote hata CHADEMA wakihitaji ushauri wangu waniite.

Nawapenda sana Wanachadema, bado tupo pamoja katika kujenga Demokrasia hata kama sipo CHADEMA.

Nawatakieni sikukuu njema za Krismas na Mwaka mpya.

Mwisho

--
Taarifa nyingine
Wakati huo huo Katibu wa Kanda ya Pwani, Casmir Mabina amejiuzulu nafasi yake baada ya kuwasilisha barua makao makuu ya CHADEMA.

Casmir ni huyo aliyekaa na Sumaye kwenye picha.
 
For the English Audience
Days after losing his position as Party Chairman for the Pwani region, Former Prime Minister Fredrick Sumaye announces that he is no longer a member of the opposition party.

In a press conference held today, Sumaye told reporters he joined CHADEMA to strengthen the opposition. He goes on saying he was welcomed warmly and it is the people that insisted he runs for Chairperso position in Pwani.

The Former PM expresses his disappointment in CHADEMA and adds that he is no longer a member of CHADEMA and will not be joining any other political party.

He has insisted that he is willing to work with all parties regardless, including Chadema. Apart from Sumaye, Casmir Mabina has also resigned his position as Chadema Coast Zone Secretary.

Commenting on this, many have pointed out that the best move for Sumaye moving forward would be for him to return to CCM. Others have expressed that there is no democracy in CHADEMA, even calling Mbowe a dictator.

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,433
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,433 2,000
Waiting kumsikiliza atazungumzia nini, japo dalili zinaonesha lazima atalalamikia uchaguzi aliopigwa chini ndani ya CHADEMA, coz source ya taarifa zinazomuhusu yeye Sumaye zinatolewa na mwanahalisi, ile ya wale jamaa waliounda kambi yao kumdhuru Mbowe, nadhani na yeye atakuwa nao kundi moja, mipango yao huwa fake sana, ina_backfire mapema!

Sumaye vipi unaenda kumshambulia Mbowe direct, tukisema umetumwa kusema ulichosema ili Mbowe aonekane mbaya mpate sababu ya kumshughulikia na msajili wenu tutakuwa tumekosea?, kwani Sumaye una 'immunity' gani lazima ushinde uchaguzi mzee, matokeo mengine huyajui, kama kushindwa!, demokrasia unayodai ilikufanya uchukue form ya uenyekiti, ndio hiyo hiyo iliyofanya ushindwe kwa kura, au kwa sababu ulikuwa peke yako ukajua lazima ushinde, basi ulikosea!

Unajinasibu kwamba ulipochukua form ya kugombea uenyekiti taifa uliwaambia wajumbe wakifanya wanachotaka kufanya utauthibitishia umma kwamba CHADEMA hamna demokrasia, but hujasema kitu gani walichotaka kufanya, sasa hapo ulikuwa na lengo gani, kuwaambia tu au kuwatisha wakuache, nao wamekuonesha hawatishiki, wakakutosa!, take a rest mzee wangu.

Kwa nionavyo huu mchezo, CHADEMA hawatayumbishwa, watamuweka huyo huyo msiemtaka, best option kwenu ni kukifuta tu hicho chama kama mtaweza!

Kwenye hili sasa ninaamini hakika Mbowe anawindwa sana, ndani na nje ya chama anachokiongoza, but kiongozi jasiri siku zote huvuka vikwazo,kama alivyokwisha onesha.
 

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Messages
8,693
Points
2,000

technically

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2016
8,693 2,000
Hana Jipya kwenye siasa za Tanzania akafie mbele alizoea kubebwa CCM miaka yote akajifunze kwa mwenzie pinda kawa waziri mkuu miaka 8 lakn amejipumzikia tu wewe miaka 10 bado unataka cheo cha mwenyekiti tena chama pinzani?.

Uyu alikuja chadema kimkakati kumzuia Lowassa asiende Ikulu.
 

papason

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Messages
3,209
Points
2,000

papason

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2010
3,209 2,000
Ila alichofanyiwa CHADEMA hakikuwa sahihi, pamoja na madhaifu yake kama alikuwa hatakiwi aenge elezwa tuu na si kudhalilishwa namna ile, ni kweli CHADEMA tuna hasira kweli kweli na 'dola' lakini haikuwa sahihi kumbwagia hasira zetu Sumaye.
 

Forum statistics

Threads 1,392,196
Members 528,564
Posts 34,101,250
Top