Freeman Mbowe arejesha fomu ya kuwania uenyekiti akimtaka Tundu Lissu kuwania Makamu Mwenyekiti CHADEMA

DAT BOY SU

Member
Nov 15, 2017
29
30
Leo huko jijini Arusha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mh. Freeman Mbowe amerejesha fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani CHADEMA.

Mh Mbowe amerejesha fomu hiyo aliyochangiwa na kuchukuliwa na vijana wa chama chake yenye thamani ya 1 million kwa Katibu wa chama hicho kanda ya Kaskazini ndugu Amani.

Wakati wa kurudisha fomu hiyo walisikika vijana na wanachama waliokuwepo katika kuhudhulia tukio hilo wakisema "Mbowe tano tena tuvushe" huku wakimshangilia kwa makofi na vigelele.

Mh mbowe aliambatana na baadhi ya wabunge wa chama hicho Mh. Halima Mdee Mbunge wa Kawe, Godbless Lema Mbunge wa arusha na baadhi wa wabunge wengine.

Katika hatua nyingine Mh. Freeman Mbowe akiongea wakati wa kurudisha fomu hiyo amemtaka au ameonea itapendeza kama aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ndugu Tundu A. Lissu kama na yeye agombee nafasi ya umakamu mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani.

Mbunge wa Arusha mijini Mh Godbless Lema na Mbunge wa Rombo Mh. Joseph Selassin nao wamekuwa katika upinzani mkubwa katika kugombea uenyekiti wa chama hicho wa kanda hiyo ya Kaskazini.
 
Tunataka demokrasia nchini ila sio ndani ya chama chetu walisikika CHADEMA wakisema.
 
Back
Top Bottom