Mwenyekiti wa CHASO - UDOM yuko mahabusu wiki ya pili sasa kwa kosa la kuwashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunga na CHADEMA

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,257
2,000
Mwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.

Kwa mujibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa CHADEMA na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

FB_IMG_1575180605460.jpg
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,989
2,000
Jiwe anaogapa hata Kivuli chake. Mwanaume gani mwoga hivyo yupo Nyuma ya Majeshi muda wote?
Watanzania, hakika hakuna aliye salama. Amkeni sasa!
 

Range rover

Senior Member
Nov 22, 2016
188
250
Kupitia jela kwa mwana cdm ni kama kufanya tambiko au kutawazwa au kusimikwa au kujitoa kafara baada ya hapo ndio unakuwa umeiva tayari kwa kuliwa.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,984
2,000
Mwenyekiti wa CHASO-UDOM bwana HENRY MANG’ERA yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na Chadema chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.

Kwamjibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa Chadema na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

1575189788803.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom