Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,316
- 24,181
Ni kiherehere changu tu kujiuliza swali la kimsingi kabisa la demokrasia ndani ya CHADEMA. Mimi si mwanachama wa chama hiki cha upinzani lakini ndio chama rasmi kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni.
Sasa hivi CHADEMA wamo katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kati ya vinyang'anyiro ni uchaguzi wa Mwenyekiti. Kati ya majina yanayofikiriwa ni kumrudisha tena kwa mara nyingine Freeman Mbowe.
Huu ni usultani! Huwezi kuendesha demokrasia kwa kuwa na Mwenyekiti yule yule, timu ile ile, na uongozi ule ule katika upinzani, halafu tukajidai watatetea demokrasia ya nchi. Kama CHADEMA hawawezi ndani ya chama chao kurekebisha katiba kuweka ukomo wa uenyekiti, mtu anajiuliza kwa Taifa je? Si ni yale yale?
Kimsingi kutobadilisha katiba ili kuweka ukomo wa madaraka sababu yake ni kuendeleza ulaji. Wakati CCM wamebadili wenyeviti mara kadhaa ndani ya miongo miwili, upinzani majina ni yale yale; Mbowe, Maalim Seif n.k.
Dhana ya demokrasia haionekani ndani ya vyama vya upinzani. Ni unafiki kufikiri watatetea katiba mpya kitaifa pindi wakipata madaraka.
=====
Maoni ya wachangiaji
(MODS hapa mmeingilia uhuru wangu wa maoni. Ieleweke na wachangiaji kuwa hii quote sijai attach mimi)

Mkuu naomba utofautishe matakwa ya katiba yaliyopo katika vyama tofauti vya siasa. Kila chama kina mila na desturi zake katika uendeshaji wake ili likapate kufikia malengo yake yaliyowekwa na itikadi kinayoisimami.
Huwezi kufananisha uendeshaji wa masuala ya kichama yaliyopo ndani ya vyama kwa kuingalia CCM kama role model katika mazingira ya kisiasa yaliyopo hivi sasa. TANU yenyewe katika uchanga wake kiliongozwa na Mwl. Nyerere kwa muda mrefu tu.
Kwa hiyo basi vyama hivi vilivyoanzishwa miaka ya 1990's bado vinahitaji "nurturing" kupitia viongozi wazoefu kutokana na changamoto zilizopo. Kwa hiyo basi bado CHADEMA inamuhitaji Mh. Mbowe katika nafasi hiyo ili kisiweze kuwa "derailed" na rafu za kisiasa zilizopo hivi sasa.