CHADEMA haijawahi na haitakuja kutokea kuwa tishio kwa CCM

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
CHADEMA wanatengeneza maneno kuwa CCM inamuogopa Mhe. Mbowe na CHADEMA ndio maana anapingwa asigombee tena.

Hii si kweli na ni upotoshaji mkubwa sana, chama chenye wasomi, wataalamu na manguli wa siasa Tanzania kiogope chama ambazo hakina mbadala zaidi ya ‘DJ’?

Toka kuanzishwa kwa CHADEMA mpaka sasa CCM haijawahi kutishika na uwepo wa CHADEMA hata kidogo. Kwa nini CCM haina hofu?

- CCM ni kikongwe kwa umri kuliko CHADEMA, wahenga wanasema ‘uzee dawa’ na CCM kuwepo muda mrefu madarakani ni tishio kwa upinzani kuiogopa CCM.

Tumekuwepo madarakani muda mrefu kwa uchaguzi wa kidemokrasia(huru na haki) na tumeshiriki CHAGUZI zote kwa amani na utulivu kwa kushirikisha wadau wote.

Uzee wa CCM umetoa fursa adhimu sana wa kupata uzoefu wa kukabiliana na changamoto nyingi, hii imetoa nafasi ya CCM kuendelea kutegemewa na kupendwa na watanzania.

- CCM ni chama cha ukombozi chenye sera madhubuti za kumkomboa mtanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kupitia ilani ya CCM tunaona ni nini CCM inapanga kufanya na tathmini ya ilani inayofanywa kila baada ya muda unabainisha sera za CCM zinatekelezeka kutokana na utekelezaji wake kufikia asilimia zaidi ya 92 mpaka sasa.

CHADEMA hakina sera zinazotekelezeka na watanzania hawajaona ahadi zilizotolewa na upinzani zikitekelezwa kwa walau 30%, hii inamaanisha kuwa sera za upinzani hazitekelezeki. Kwa ‘ logic’ hiyo, CHADEMA inawezaje kuwa tishio kwa CCM?

- CCM hakina mbadala lakini wanaCCM wanambadala na ndio maana toka 2014 mpaka sasa CCM imepata kuwa na wenyeviti watatu.

CCM kina muundo mzuri wa kuchaguana na kuteuana nafasi mbalimbali za Chama na kila mwanachama na uhuru na haki sawa na mwingine katika nafasi yeyote ndani ya chama.

Tofauti na CCM, CHADEMA kina mbadala( inaweza kuwa CUF, ACT, n.k.) lakini wanaCHADEMA hawana mbadala ndio maana tunaona ndani ya miaka 15 toka 2014 kina mwenyekiti mmoja tu wa kudumu na hakuna uhuru, haki na usawa baina ya wanachama kwa baadhi ya nafasi ndani ya chama.

Chama kutokuwa na mbadala ni jambo linalowezekani lakini mwanachama kutokuwa na mbadala ni hatari kwa afya ya demokrasia na siasa za ushindani wa hoja.

WanaCCM na watanzania wengine wote wanachotaka kuona CHADEMA inafanya ni kile chenye kutia matumaini na hofu ya kutawaliwa ‘kisultani’ kwa sababu amekosekana mwanachama mbadala wa kuongoza chama, je Chama hiki akitasema kimekosa mtu wa kuongoza nchi kikishika madaraka na kumuweka kiongozi madarakani maisha?

Hakuna sehemu CCM inapoingilia uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kwa sababu CHADEMA haijawahi na haitakjuja kutokea kuwa tisho kwa CCM.

Linapokuja suala la Tanzania, wanachama wa vyama vingine wana haki ya kusema na kuonya kwa sababu lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola na lisipokemewa, yanayofanyika ndani ya chama yatafanyika ndani ya nchi na asitokee mtu wa kukemea tena nchi inapoangamia.

Tanzania ni yetu sote.
 
..but ccm is not taking any chances.

..na inatumia polisi, usalama wa taifa, na mahakama, kuwakandamiza cdm na vyama vingine vya upinzani.
 
....kweli hamumuogopi, ila zile risasi mlizomkosa nazo pale Mkwajuni na kule Soweto Arusha sijui mlikuwa na lengo gani nae!, au mlikuwa mnamfanyia upako wa aina ya kipekee?!
 
Ingekuwa ccm haigopi Chadema basi wangeweka ulingo sawa,haya kuzuia watu wasifanye siasa,kutisha watu,kupokonya demokrasia ya uchaguzi yanini kama kweli hamna hofu.
 
Back
Top Bottom